Vitu vya kuzingatia kabla ya kuacha kazi

Vitu vya kuzingatia kabla ya kuacha kazi

nyabaheta

JF-Expert Member
Joined
Dec 4, 2012
Posts
247
Reaction score
82
Habari wakuu,mimi ni mwajiriwa mahala flani lakini pia namind business zangu,sasa natamani sana kuacha kazi ili nimind my own business kwa uhuru na nipate muda wa kutosha kukaa na familia yangu,naomba ushauri wa vigezo gani nizingatie hapa au nisubiri business ikue ifike level gani ndo nipige chini hii day job.

Sent from my BlackBerry 8520using JamiiForums
 
Zingatia kama utaweza kuzikabili changamoto za kujiajiri.
 
Muhimu kuwa na uhakika wa kuipa familia yako mahitaji muhimu kwa mwaka mzima, hata kama biashara yako itaenda kombo...

Ili ukiona mambo yamegoma kabisa urudi kwenye mapambano ya kusaka ajira huku familia haitetereki na baba kuacha kazi...
 
Michango mizuri wakuu.

Sent from my BlackBerry 8520 using JamiiForums
 
1.uwe na biashara inayokuingizia kipato kila siku 2.uwe na fixed assets km nyumba angalau mbili tatu.
 
Binafsi sioni kama nyumba za kawaida za kifamilia kama zinaweza kukufanya mtu uishi vizuri maana rent yake na matunzo utaona kinachobaki ni kidogo tu.

Anzisha miradi midogo midogo zaidi ya mmoja, kwani miradi midogomidogo hulipa zaidi na gharama za uendeshaji ni nafuu kuliko miradi mikubwa itakuumiza kichwa na pengine hata kukutifulia mipango yako tokana na ughali wa uendeshaji wake.

Miradi midogo midogo utakuwezesha kujenga nyumba unazokusudia baadaye kwa mwendo pole lakini kwa uhakika. Binafsi sioni sababu ya kuweka pesa zote kwenye majengo kwani si rahisi majengo kukupatia mara moja kiwango unachotaka labda kwa utaratibu wa mikopo majengo yakiwekwa rahani na hapo biashara ikigoma basi ujue majengo umeyatelekeza kwa wahasimu wako mabenki.
 
1. Ongea na familia yako kuhusu mpango wa kuacha kazi, waambie ni kwa nini unaacha kazi na umuhimu wa kuwa mjasirimali

2. Anza maandalizi ikiwemo kuwa na biashara yako ambayo itakusaidia kuendesha maisha

3. Anza practical mfano: unaweza chukua likizo na ukafanya practical ya wewe kuwa full katika biashara yako

4. Hakikisha biashara yako ni sustainable na si ya ubabaishaji, hakikisha umeisha ifanyia research ya kutosha

5. Anza kwa kuanza kuachana na baadhi ya marafiki ambao unaona watakwamisha safari yako, mfano marafiki wenye mwelekeo wa kazi sana, tafuta marafiki wenye mwelekeo wa kujijiri ndo wawe marafiki

6. Muda wako, mawazo yako yajikite zaidi katika kujiajiri mwenyewe,

7. UKISHA KAMILISHA HAYA MKUU, UNAWEZA ANZA KUAGA KAZINI, HAKIKISHA UNAWAAGA WENZAKO

MWISHO CHOMA MELI MOTO AU FANYA ALICHO AGIZWA RUTU KUFANYA WAKATI ANAONDOKA SODOMA NA GOMORA
 
Acha kazi faster then pambana na changamoto za kujiajiri. I mean liwalo na liwe ndo mpango mzima..!
 
Back
Top Bottom