Jamani mnipe ushauli,mimi nina mpenzi wangu nimekaa naye almost 2year mara nilimheshimu kama mume wangu mtarajiwa tangu hapo tulipoanza lakini siku zote uchumba ulishamiri na hatimaye aliniambia tuwaambie wazazi mi nikawaeleza home lkn bse yeye yupo chuo 2nd year tulikubaliane amalize shule ndipo tufunge ndoa ambapo ni mwakani lkn sasa vituko vimeanza kabla ya yote juzi mdada mmoja alinitumia sms akisema huyo ni mchumba wake niachane naye kwa busara nilimjibu huyo dada asijali nitamwachia tu kwani sipendi kugombania mwanaume baadaye nikampigia mhusika akasema sio kweli nikamuuliza hiyo namba unaijua akasema ndio ni rafiki yake wanasoma pamoja discussion mbaya zaidi nikapiga tena muda mwingine akapokea mdada akasema mwenye simu yuko anaoga, kweli niliishiwa nguvu kupiga tena simu imezimwa tena usiku mzm kufunguliwa asub hayo majibu ninayopewa ya mkato tu kwanza hataki kuongea nami,yaani ni vituko tu kinachoniuma nilimpatia laptop yangu aitumie chuoni nikijua namjenga mume wangu sasa nikimwambia naomba laptop ananijib vibaya hapa nilipo sijui la kufanya kweli nilimpenda lkn kwa vituko hivi nipo njia panda