Vituko jikoni, Let us share and have fun

Vituko jikoni, Let us share and have fun

Niliwahi kupika wali nikajaza sufuria maji ili uchemke na kuiva vyema!!!! Kilichotokea ni matope halafu siku hio nikaachiwa nyumba, kidume nikaamua nijipikie chips nifaidi duh! Hadi leo nimeachana na biashara ya kupika naona sio fani yangu
 
Na vile viungo vingine ambavyo inabidi uweke kwenye pilau, vingine inabidi utwange. Nikifikiria zoezi lote hili basi hata ile tamaa ya kujaribu inapotea

BAK katika upishi rahisi ni pilau kama la kuku ambae si mgumu kuwiva within 1 hour tayar kwa kuliwa.. . Yaani nikiwa na haraka zangu na lazma nipike basi upishi rahisi niunao ni pilau
 
Na vile viungo vingine ambavyo inabidi uweke kwenye pilau, vingine inabidi utwange. Nikifikiria zoezi lote hili basi hata ile tamaa ya kujaribu inapotea

Haiko ngumu hivo jaribu bhana
 
Hahahaha pole J C

Asante sana. Jamaa alikuwa baunsa ni Nouma alafu alikuwa anafanya boxing nikaishia kuwa mpole kiheshimiwa zaidi na tai shingoni. Zaidi ya hapo sijawahi shindwa lolote katika mapishi.
 
Last edited by a moderator:
Niliwahi kupika wali nikajaza sufuria maji ili uchemke na kuiva vyema!!!! Kilichotokea ni matope halafu siku hio nikaachiwa nyumba, kidume nikaamua nijipikie chips nifaidi duh! Hadi leo nimeachana na biashara ya kupika naona sio fani yangu

Hata chipsi mayai pia? Kuna mmoja alipika chipsi mayai si akataka kugeuza kwa sahani kama wanavyogeuza wauza chipsi weee wakat anageuza si mafuta yamdondokee mkononi mana aliweka mafuta mengi hahaha chipsi pindu zote zimeanguka chini ba alikua ana njaa aliliaje.....
 
Asante sana. Jamaa alikuwa baunsa ni Nouma alafu alikuwa anafanya boxing nikaishia kuwa mpole kiheshimiwa zaidi na tai shingoni. Zaidi ya hapo sijawahi shindwa lolote katika mapishi.

Hahahaha jamani.....saivi ina maana wewe chef wa ukweli?
 
Hahahahahaha lol!!!! Chuzi la Maji special made by Chef Mrs Kharusy!!!!

Nilivyokua 11-12yrs khaloo yangu alitualika kwake bahati mbaya ukweni wakafiwa ikabidi atuachie jiko tupike wenyewe maagizo ilikua tupike wali wa nazi na mchuzi wa maji, tulikua na mke wa my uncle nae alikua sifuri kwenye upishi...doh..ati ananiuliza mm wat to do na mm enzi hizo hata jikoni siingii loh tukaufurumusha wali ukatoka bondo ilimradi umewiva...huo mchuzi sasaa tena wa maji aunty ananiuliza unapikwaje nikamwambia weka mafuta kaanga kitunguu na tungule halafu mimina na maji ...looh mhuuu ,tukafanya hivyo wenye nyumba wamerudi wanashangaa chuzii chururuuu linang'aa mafuta... tukaulizwa ndo wa maji huu??! tukasema si ndio mumetaka mchuzi wa maji!!!
 
Last edited by a moderator:
Na vile viungo vingine ambavyo inabidi uweke kwenye pilau, vingine inabidi utwange. Nikifikiria zoezi lote hili basi hata ile tamaa ya kujaribu inapotea

Alafu ilo chuzi lako hebu tuekee recipe siku moja tujirambe na sie
 
Du!. Acha niende kununua Nazi nikaiandaa vema na mchele nusu . Bwabwa likaiva haswa nikaliacha jikoni vizuri ili nipumzike kidogo kwa badae kui enjoy wa Nazi. Ajaja jamaa mmoja huwa tunamwita kaka pindi hicho anaishi home katoka huko na njaa mbaya kafikia jikoni acha aji servie akaukomba wote hadi kukokoa ukoko. Naamka naenda jikoni nakuta sufuria empty kuuliza naambiwa jamaa kala du iliniuma sana mpaka wa Leo rafiki zangu wakiniona wanacheka sana huku wakisema WA NAZI wakirefer msosi wangu ulioliwa . Du!.

Hahahaaa...umenikumbusha kuna siku nilipika wali wa nazi, shurti wali unanukia, tui zitoooo na maharage ya nazi matamuuuu....ule msosi hata kuuonja nliona shida...nliogopa kushiba jikoni...nilipanga nile nivimbiweee....

Basi wamekuja mashost, si nikawasindikiza huku nimepalia wali wangu jikoni....story story nikachelewa kurudi....Daadeki mama kakasirika....wakapakua wenyewe chakula....yani hadi makoko....wakaacha sufuria nyeupeee kama imeoshwaaaa.....jamani nilinunaaaaa!
 
Kuboronga besti...

Ila hio ya ugali hongera...mm hata wa peke yangu sijawahi na sijapanga siku ya kujaribu as long as wataalam wapo...lol

Yani mpaka nimejua kusonga ugali...nyumbani nishawalisha masotojo ya kila aina....mpaka leo nikitaka kusonga ugali bro wangu ananambia uji ukichemka nimuitee....hawaniamini....!

Ila siri ya ugali mzuri uji uchemkee uive na usiwe mwepesi sanaaa!
 
Mrs Kharusy siku yako ya kwanza kupika mikate ya maji ilikuaje? Upishi ulinipa shida ule

Hahhahah lol.....sikumbuki bt must be shapeless na kukatikakatika kwenye kugeuza... zamani tulikua tunaachiwa ya mkate wa mwisho kujaribu (esp ramadhan) kisha uule mwenyewe lol
 
Last edited by a moderator:
Hahahaaa...umenikumbusha kuna siku nilipika wali wa nazi, shurti wali unanukia, tui zitoooo na maharage ya nazi matamuuuu....ule msosi hata kuuonja nliona shida...nliogopa kushiba jikoni...nilipanga nile nivimbiweee....

Basi wamekuja mashost, si nikawasindikiza huku nimepalia wali wangu jikoni....story story nikachelewa kurudi....Daadeki mama kakasirika....wakapakua wenyewe chakula....yani hadi makoko....wakaacha sufuria nyeupeee kama imeoshwaaaa.....jamani nilinunaaaaa!

Du!. Pole sana. Mtembezi hula miguu yake. Teh Teh Teh!
 
shangazi yangu toka bara huko, mjomba alitoka pwani na nazi akafika pale na kipeto cha mchele na nazi kadhaa akatua mzigo kwasababu ya kiu akasema tutaongea baadaye ngoja nikapate kwanza komoni/pombe ila alimwambia shangazi kuwa nimekuletea mchele na nazi viko humo. alipoondoka tu shangazi kafungua kipeto alichoonyeshwa kuletewa nazi, akachukua mchele na kuchambua na kuupika ili kumfanyia saprise mjomba namna anavyojua kupika kwa nazi akapasua na kuyaweka yale maji ya madafu. jioni mjomba kurudi analetewa ubwabwa na shangazi anamwambia nimeweka na ile nazi. kula mjomba kasema mbona kama hamna iyo nazi?akasema nimeweka, kauliza makokwa yako wapi? akasema nimeshatupa nje, kwenda kuyachukua hajakuna nazi wala nini.alijua labda yale maji ndio ya kuungia.

Ha ha haaaaaaaa, noma aiseee. Umenivunja mbavu.

Mi kuna sister wangu mmoja alikutwa anaosha samaki kwa sabuni eti kila akiwaosha hawatoki shombo. Lol
 
Ha ha haaaaaaaa, noma aiseee. Umenivunja mbavu.

Mi kuna sister wangu mmoja alikutwa anaosha samaki kwa sabuni eti kila akiwaosha hawatoki shombo. Lol

Sister wangu yeye akiambiwa osha samaki mbio anaenda vaa buibui na kutokaanasema wana discussion shuleni daily ndie zake hadi tukamshtukia. ..

Siku nyumbani jioni.wameletwa pweza basi nkaambiwa niwaoshe alafi niweke kwa freezer bibi mie nkajitia pirika weee sikutaka kuwaosha nkaenda kulala saa nne nkaja amsha na mama ananiambia hulali ntamwaga maji kitanda chako kama hutawakosha loh ile ndo niko waosha na ndo natoka usingizi ilikua usiku kila nkijaribu kuosha naogopa pweza wanatisha ni wakubwa sana loh nkapiga kelele mama akaja nsaidia binafsi pweza likiwa kubwa sana huo namuogopa kumkosha ila akiwiva siogopi kulaaa hahaha mroho mie lol
 
Umenikumbusha mbali, siku moja eti nilijifanya nawasaidia kazi ya kupika nyumbani kwangu. nilimwambia mke wangu, na watoto kwamba leo nataka niwapikie msosi ili mjue nasisi wanaume tunajua kukaangiza sana. hivyo niliwaambia anaye taka kukaa jikon akae asiye taka afanye shughuri zake vikiiva mtaitwa. niliwaambia waniandalie kila kitu jikoni. Nilichagua kupika chips na kukaanga kuku + kachumbari. mambo yalikwenda vizuri wao wakiwa seburin wanasubilia surprise ya msosi wa baba, mtoto wangu mdogo alikuja jikoni kucheza kumbe alimwaga mafuta ya kula chini kwenye tails, mimi sikuona.

nilipika chips vizuri na kuku, mwishoe nikamalizia kuwatengenezea kachumbari, nikiwa nimeshika sahan iliyo shehen kachumbari nilikanya yale mafuta kwenye tails bila kujua, na hivyo nikateleza na kuanguka vibaya jikoni na kachumbari yangu ikamwagika. ilinibidi ninyanyuke fasta kabla hawajaniona na house girl asije kunicheka kwamba baba mwenye kaya kaanguka jikoni!!!! mototo wangu wa kike alikuja na kusema baba nimesikia kitu kinalia sana PUUUUU, ni nini? nilimwambia nimeanguka mwanangu ila nyamaza usiwaambie wenzio. hivyo akafanya usafi wa yale mafuta na kachumbari. akanisaidia kutengeneza nyingine. tulipo kuwa tunakula nilitamani niwaambie ila nikaona aibu nikaja kumwambia wife chumbani mwenzio nimepiga mweleka. mpaka leo sitamani hata kukatisha katisha jikoni!!!
 
Vyakula ambavyo sitaki kujifunza kupika ni chapati, pilau na vyote vya kukanda unga. Process yake ni ndefu sana ila navipenda sana kuvila lol!!!! Kisa cha kusukuma chapati 20 shapeless kama za Mkuu Bulldog lol! . Ndizi za kupika poa ila zinaniudhi kumenya. Mikate ya maji kama kawa. Mie dingi haoni noma kuingia jikoni kutengeneza kile akitamanicho kula nami sioni noma yoyote kwenye hii idara. Like father like son.

Sisi kwetu wanaume wote, na kipindi tulivyokuwa shule tukirudi likizo hausgel anaenda likizo, kazi zote tulikuwa tunafanya sisi. Muda mwingi bi mkubwa akipika unatakiwa uwepo pale ukichukua maujuzi, au anaweza kusafiri ukabaki na wadogo zako na wanatakiwa kula. So far, nimeenjoy kujifunza na kujua kupika.
 
Back
Top Bottom