shangazi yangu toka bara huko, mjomba alitoka pwani na nazi akafika pale na kipeto cha mchele na nazi kadhaa akatua mzigo kwasababu ya kiu akasema tutaongea baadaye ngoja nikapate kwanza komoni/pombe ila alimwambia shangazi kuwa nimekuletea mchele na nazi viko humo. alipoondoka tu shangazi kafungua kipeto alichoonyeshwa kuletewa nazi, akachukua mchele na kuchambua na kuupika ili kumfanyia saprise mjomba namna anavyojua kupika kwa nazi akapasua na kuyaweka yale maji ya madafu. jioni mjomba kurudi analetewa ubwabwa na shangazi anamwambia nimeweka na ile nazi. kula mjomba kasema mbona kama hamna iyo nazi?akasema nimeweka, kauliza makokwa yako wapi? akasema nimeshatupa nje, kwenda kuyachukua hajakuna nazi wala nini.alijua labda yale maji ndio ya kuungia.