Determinantor
Platinum Member
- Mar 17, 2008
- 59,045
- 94,974
BAK katika upishi rahisi ni pilau kama la kuku ambae si mgumu kuwiva within 1 hour tayar kwa kuliwa.. . Yaani nikiwa na haraka zangu na lazma nipike basi upishi rahisi niunao ni pilau
Na vile viungo vingine ambavyo inabidi uweke kwenye pilau, vingine inabidi utwange. Nikifikiria zoezi lote hili basi hata ile tamaa ya kujaribu inapotea
Niliwahi kupika wali nikajaza sufuria maji ili uchemke na kuiva vyema!!!! Kilichotokea ni matope halafu siku hio nikaachiwa nyumba, kidume nikaamua nijipikie chips nifaidi duh! Hadi leo nimeachana na biashara ya kupika naona sio fani yangu
Asante sana. Jamaa alikuwa baunsa ni Nouma alafu alikuwa anafanya boxing nikaishia kuwa mpole kiheshimiwa zaidi na tai shingoni. Zaidi ya hapo sijawahi shindwa lolote katika mapishi.
Nilivyokua 11-12yrs khaloo yangu alitualika kwake bahati mbaya ukweni wakafiwa ikabidi atuachie jiko tupike wenyewe maagizo ilikua tupike wali wa nazi na mchuzi wa maji, tulikua na mke wa my uncle nae alikua sifuri kwenye upishi...doh..ati ananiuliza mm wat to do na mm enzi hizo hata jikoni siingii loh tukaufurumusha wali ukatoka bondo ilimradi umewiva...huo mchuzi sasaa tena wa maji aunty ananiuliza unapikwaje nikamwambia weka mafuta kaanga kitunguu na tungule halafu mimina na maji ...looh mhuuu ,tukafanya hivyo wenye nyumba wamerudi wanashangaa chuzii chururuuu linang'aa mafuta... tukaulizwa ndo wa maji huu??! tukasema si ndio mumetaka mchuzi wa maji!!!
Na vile viungo vingine ambavyo inabidi uweke kwenye pilau, vingine inabidi utwange. Nikifikiria zoezi lote hili basi hata ile tamaa ya kujaribu inapotea
Alafu ilo chuzi lako hebu tuekee recipe siku moja tujirambe na sie
lol!!! Sijakufikia weye wala sitakufikia wewe ni Expert.
Aibu kwenye kuboronga? au kwenye nini?
Du!. Acha niende kununua Nazi nikaiandaa vema na mchele nusu . Bwabwa likaiva haswa nikaliacha jikoni vizuri ili nipumzike kidogo kwa badae kui enjoy wa Nazi. Ajaja jamaa mmoja huwa tunamwita kaka pindi hicho anaishi home katoka huko na njaa mbaya kafikia jikoni acha aji servie akaukomba wote hadi kukokoa ukoko. Naamka naenda jikoni nakuta sufuria empty kuuliza naambiwa jamaa kala du iliniuma sana mpaka wa Leo rafiki zangu wakiniona wanacheka sana huku wakisema WA NAZI wakirefer msosi wangu ulioliwa . Du!.
Kuboronga besti...
Ila hio ya ugali hongera...mm hata wa peke yangu sijawahi na sijapanga siku ya kujaribu as long as wataalam wapo...lol
Mrs Kharusy siku yako ya kwanza kupika mikate ya maji ilikuaje? Upishi ulinipa shida ule
Hahahahahaha lol!!!! Chuzi la Maji special made by Chef Mrs Kharusy!!!!
Hahahaaa...umenikumbusha kuna siku nilipika wali wa nazi, shurti wali unanukia, tui zitoooo na maharage ya nazi matamuuuu....ule msosi hata kuuonja nliona shida...nliogopa kushiba jikoni...nilipanga nile nivimbiweee....
Basi wamekuja mashost, si nikawasindikiza huku nimepalia wali wangu jikoni....story story nikachelewa kurudi....Daadeki mama kakasirika....wakapakua wenyewe chakula....yani hadi makoko....wakaacha sufuria nyeupeee kama imeoshwaaaa.....jamani nilinunaaaaa!
shangazi yangu toka bara huko, mjomba alitoka pwani na nazi akafika pale na kipeto cha mchele na nazi kadhaa akatua mzigo kwasababu ya kiu akasema tutaongea baadaye ngoja nikapate kwanza komoni/pombe ila alimwambia shangazi kuwa nimekuletea mchele na nazi viko humo. alipoondoka tu shangazi kafungua kipeto alichoonyeshwa kuletewa nazi, akachukua mchele na kuchambua na kuupika ili kumfanyia saprise mjomba namna anavyojua kupika kwa nazi akapasua na kuyaweka yale maji ya madafu. jioni mjomba kurudi analetewa ubwabwa na shangazi anamwambia nimeweka na ile nazi. kula mjomba kasema mbona kama hamna iyo nazi?akasema nimeweka, kauliza makokwa yako wapi? akasema nimeshatupa nje, kwenda kuyachukua hajakuna nazi wala nini.alijua labda yale maji ndio ya kuungia.
Ha ha haaaaaaaa, noma aiseee. Umenivunja mbavu.
Mi kuna sister wangu mmoja alikutwa anaosha samaki kwa sabuni eti kila akiwaosha hawatoki shombo. Lol
Vyakula ambavyo sitaki kujifunza kupika ni chapati, pilau na vyote vya kukanda unga. Process yake ni ndefu sana ila navipenda sana kuvila lol!!!! Kisa cha kusukuma chapati 20 shapeless kama za Mkuu Bulldog lol! . Ndizi za kupika poa ila zinaniudhi kumenya. Mikate ya maji kama kawa. Mie dingi haoni noma kuingia jikoni kutengeneza kile akitamanicho kula nami sioni noma yoyote kwenye hii idara. Like father like son.