Vituko jikoni, Let us share and have fun

Vituko jikoni, Let us share and have fun

Kuna siku nilikuwa napika kachori nikaandaa kila kitu. Kwenye unga sasa, si nikakosea nikachovea vile viazi na unga wa sembe!! Bila hata kushtuka nkaanza kuchoma kachori zangu, nkashangaza zinapukutika mle kwenye karai yaani vile viazi havishikani na unga!tahamaki ndo nagundua ninechanganya mifuko ya unga.halafu ilikuwa ramadhani na kijua kishazama.uzuri nilikuwa peke yangu.....kwa muda nlopoteza nkaamua kwenda kujinununulia "tokoro" za mama ntilie wa ughaibuni.lol sitasahau!
 
Hahahahaha pole shoga angu umejua kunchekesha
 
Pindi najifunza kupika Ugali, si nikapika mbichi, manake niliweka unga hata maji hayajachemka. We nilichokifanya ni kutupa batini kabla mtu hajaona Halafu nikaanza upya!!

Mie kwenye kupika ugali nimeharibu unga balaa. Nilikua Sijui kukorogea wala kusubiri maji yachemke, najaza miunga tu, nikiula mbayaaa nautupa. Ilifika point mama akachoka kuninyamazia.... nilikula ugali mbichi na fimbo juu.
 
hii ilinikuta mimi nikiwa napika wali na umeme umekatika ghafla kabla sijaweka mafuta, kushikashika kwenye giza nikadhani ni kopo la mafuta kumbe majani ya chai. nikawa na wasiwasi na nilichotia kwenye wali, nikatafuta karatasi ili niwashe nichungulie nilichotia, loooh! kumbe majani ya chai. nilichukua sifuria faster nikamwaga wali wote chooni kabla mama hajanikuta nikaanza upya na uzuri wake mchele upo ndani. Loh!

[emoji23][emoji23][emoji23][emoji23][emoji23]
 
Niliachwa home siku moja nika waambia wakirudi watakuta ubwabwa na maharage shatashata, mambo yakawa mengi ratiba zikaingiliana hadi saa moja jioni sijafanya chochote.
Mungu mkubwa hakuna ambaye alikua amesharudi home, nika nunua mkaa nika bandika maharage nikawasha feni kuelekeza jikoni ili yaive faster.
Huku kwenye mchele nikatumia gesi!! sasa nilipo haribu niliweka madoido, nikataka kuweka carrot kama wanawake wanavyoweka weee...ulikua wa brown 😀 😀
 
[emoji12][emoji23]
 
na kupika uji ilikuwaga changamoto sana ,kila nikipika lazma utoke.na mabonge au mzito sana,basi.mama alikuwa ananisema sana,baba ye hajali sana mana anapenda kula,hadi nlivokuja kujua siri ya uji ni kuchemsha maji na ukishaanza kukoroga usiache hadi uive...
ingine siku moja usiku nmechoka mamma kanambia nichemshe maziwa ndo niyaeke kwenye friji,nkaweka pressure cooker,sikuifunika lakini,nkawasha jiko nkaishia zangu kulala,mama kawahi kuamka alfajiri jikoni kakuta kumejaa.moshi sufuria jeusiii,shukuru Mungu sufuria lilikuwa zito,maziwa yalichemka hady yakakauka, plate ya jiko nyekunduu jiko nilijisahau likawaka usiku.mzima...hehehehhe nilichezea kchapo sitasahau,sijui ningeunguza nyumba,thanx God the worst didn't happen..
Dingi yako alikuepo? Hakusema chochote
 
Angel Nylon siku ya kwanza kupika ugali nlimkuta mama anapika nkamwambia leo niachie mie anakambia hutaweza nkwamwambia acha tu nakumbuka niko form 2 kipindi hiko loh nkaachiwa nlijuta kumbe upishi wa ugali unataka nguvu basi nkawa nasonga naona siwezi tu ugali mwingi kama nini maana twala watu tele home mwishowe nkashindwa nkamwambia malizia ila alinipa moyo nimejitahidi.....tangu siku hiyo sikusonga tena ugali second time nasonga ugali nimeshaolewa ila hata sio mzuri kiivo hadi leo msongaji hubby wa ugali unakuajee mtamu
Wewe ni mwarabu?
 
Back
Top Bottom