Vituko jikoni, Let us share and have fun

Kuna siku nilikuwa napika kachori nikaandaa kila kitu. Kwenye unga sasa, si nikakosea nikachovea vile viazi na unga wa sembe!! Bila hata kushtuka nkaanza kuchoma kachori zangu, nkashangaza zinapukutika mle kwenye karai yaani vile viazi havishikani na unga!tahamaki ndo nagundua ninechanganya mifuko ya unga.halafu ilikuwa ramadhani na kijua kishazama.uzuri nilikuwa peke yangu.....kwa muda nlopoteza nkaamua kwenda kujinununulia "tokoro" za mama ntilie wa ughaibuni.lol sitasahau!
 

Hahahahaha pole shoga angu umejua kunchekesha
 
Pindi najifunza kupika Ugali, si nikapika mbichi, manake niliweka unga hata maji hayajachemka. We nilichokifanya ni kutupa batini kabla mtu hajaona Halafu nikaanza upya!!

Mie kwenye kupika ugali nimeharibu unga balaa. Nilikua Sijui kukorogea wala kusubiri maji yachemke, najaza miunga tu, nikiula mbayaaa nautupa. Ilifika point mama akachoka kuninyamazia.... nilikula ugali mbichi na fimbo juu.
 

[emoji23][emoji23][emoji23][emoji23][emoji23]
 
Niliachwa home siku moja nika waambia wakirudi watakuta ubwabwa na maharage shatashata, mambo yakawa mengi ratiba zikaingiliana hadi saa moja jioni sijafanya chochote.
Mungu mkubwa hakuna ambaye alikua amesharudi home, nika nunua mkaa nika bandika maharage nikawasha feni kuelekeza jikoni ili yaive faster.
Huku kwenye mchele nikatumia gesi!! sasa nilipo haribu niliweka madoido, nikataka kuweka carrot kama wanawake wanavyoweka weee...ulikua wa brown πŸ˜€ πŸ˜€
 

[emoji12][emoji23]
 
Dingi yako alikuepo? Hakusema chochote
 
Wewe ni mwarabu?
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…