Kabla ya kuwa mtaalamu jikoni lazima uboronge kwanza tena vingine hata haviliki ni vya kumwaga tu. Hongera kwa kumshawishi sister wako ajiunge hapa.
Story za kuboroga nnazo telee maana ikiwa mtu kaboronga tunamchekaa siku ya pili anakua na ari mpya lol.....
Cousin yangu last year alipika kachori aliziunga vizuri sana tu sasa wakati wa kuchoma sasa ule uji kafanya mwepesi na mafuta hayajapata moto vizuri akazitia kachori kabla ya hapo nlikua namuambia umekosea hiki nkaambia nifunge bakuli langu, weeee kachori zilitumbuka zote akabaki kukaanga uji wenziwe walimchekajeee na mie mmoja wapo lol