Grereza la Kober analoshikiliwa aliyekuwa rais wa Sudan,Omar Albashir limevunjwa na mahabusu wote kukimbia. vikundi vinavyopigana kila kimoja kinaonesha kutokuwa na uhakika wa sehemu alipo kiongozi huyo wa zamani anayetafutwa na ICC.
jeshi la Sudan chini ya generali Burhani limesema kiongozi huyo walimuhamisha mapema kumpeleka hospitali ya jeshi kweny ulinzi mkali. wakati huo huo upande wa generali Dagalo umesema jeshi hili limemtorosha ili kumrudisha madarakani.
Mmoja wa mahabusu hao wanaotafutwa na ICC aitwaye Ibrahim anasema baada ya gereza hilo kupigwa na makombora na kukosa huduma za chakula na maji ilibidi yeye na wenzake waondoke kwa ajili ya usalama wao..Hata hivyo hakumtaja Omar Albashir kuwa alikuwa miongoni mwao.Amesema yeye amependa ajisalimishe kwenye kituo chochote cha polisi lakini vituo vyote amekuta havifanyi kazi.
Video moja ya mtandaoni imewaonesha mahabusu hao wakiwa wamebeba mikoba yao kuingia mitaani baada ya gereza hilo kuvunjwa.