Vituko vya jikoni, ushawahi fanya kitu gani wakati unapika?

Nyendo

JF-Expert Member
Joined
Jun 4, 2017
Posts
1,336
Reaction score
4,731
Mko poa?

Salaam,

Jikoni kuna wakati yanatukia matukio jikoni wakati unapika mpaka unatamani unashangaa, mwenzenu nilimwaga mboga wakati napika ugenini kisa kapita panya na sikuwa najua kama nyumba ina panya.

Nimeaza kupika ile naipuka mboga Panya kakatiza nikaona mkia tu nikadhani nyoka nikaaruga mboga chini nikaanza kuwaza nifanye nini na nipo ugenini.

Mara paap akili ikaja nizoe mboga nioshe uzuri ilikuwa inaosheka, nikaanza kuzoa mara mwenyeji wangu kanikuta namalizia akaguna tu nikakosa hata cha kumwambia yeye ananishangaa mimi namalizia kuosha nikarudisha jikoni zikachemka nikaunga vizuri zikawa nzuri.

Baade nikamfata mwenyeji kumuomba msamaha kwa kumwaga mboga.

 
Nilikuwa nimetoka kazini nimechoka balaa,nikamenya viazi ili nipike chips,nilipomaliza nikaweka mafuta kwenye sufuria,nikaweka kwenye jiko la mchina,nikasema ngoja nijiegeshe kidogo kwenye kochi,usingizi ukanipitia,niliposhtuka,nyumba yote imejaa moshi,kukimbilia jikoni moto unawaka kutokea ndani ya sufuria,nikakimbilia nje kuchota michanga,bahati kulikuwa na kifusi ndio ponya yangu,nikatupia kwenye moto mpk ukazimika...
 
Kuna ka jamaa kaliweka boko boko kwa thermos aisee Watu walishinda njaa
 
Hili wengi wamefanya
 
[emoji23][emoji23][emoji23]
 
Ulionekana mchawi aisee
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…