hilo jina la Mensah alipewa akifanannishwa na kipa wa zamani wa Ghana (Robert Mensah)
hiyo mechi ya Pan na Majimaji zile fujo za pondamali na Peter Tino zilisababisha yule refa (Manyama) kukatika kidogo ulimi
nakumbka ilikuwa ni mechi kati ya Yanga na Afican Sports, pondamali alidaka mpira akamrushia strika wa Sports (Victor Nkanwa), lakini bila kutarajia Nkanwa akashindwa cha kufanya, na mara ya pili tena pondamali alirudia hicho kitendo na Nkanwa akawa makini baada ya Kuupiga kwa papara aliutuliza na kumchambua pondamali, sasa wakina Minziro na jeuri yao yote na machungu yao yote walishindwa kabisa kumgusa huyo jamaa
kwa wasiofahamu huyo jamaa ni BLACK BELT YA KARATE, alikuwa sana pale maeneo ya Zanaki enzi hizo, za kina Sensei Henry, Sempai Magoma na kina Mawala (Mzee wa Judo)