Vituko vya madereva: Wimbo wa Umoja wa Vijana Tanu na Mzee Makongoro

Bujibuji Simba Nyamaume

JF-Expert Member
Joined
Feb 4, 2009
Posts
76,107
Reaction score
160,001
Mzee Makongoro alikuwa ni mwalimu wa Kwaya ya Vijana ya TANU ambayo ilivuma Sana kwa nyimbo za asili na nyimbo zake zilipata umaarufu mkubwa Sana miaka ya sabini na themanini kupitia vipindi mbalimbali vya redio kama TUIMBE SOTE na kipindi cha TUMBUIZO ASILIA kilichokuwa kikirushwa hewani na Radio Tanzania Dar es Salaam (RTD) na kikitangazwa na hayati Michael

Your browser is not able to play this audio.
 
Ni wimbo wa Makongoro, nyimbo za Ngw'namila (Mwinamila), zilikuwa za Kisukuma.
P
Asante sana. Halafu kuna ule wimbo wa kisukuma wa mwaka 1987 Sabasaba Shinyanga. Ukulima wa kisasa balimi mwangalile kwanza malali...
Sijui kama nimepatia hayo maneno. Nadhani wa Mwinamila
 
Heshima kwako mkuu nimekubali wewe ni maji ya kina kirefu
 
Huo wimbo ulikuwa wa Mzee Makongoro kweli (siyo Ng'winamila), ambaye baadaye aligongwa na madereva hao hao aliowaimba.
 
Yaani kuja tena kuisikia hii classic imeniweka pahali yake.....nitaanza kuwapotezea....
Maana huwa wananitia hasira nakuwa na matusi njia nzima mpaka najisahau, na kuna siku nipo mama yangu mzazi kwenye gari yakanitoka matusi machafu na kushuka kutaka kumtoa mtu nyongo na bisibisi...
baadae nikajiona mjinga kabisa, sitasahau...
 
Unaendesha guta?
 
Huu wimbo umenipa raha sana. Nimekumbuka zamani
 
A real Classic tune
 
Kweli JF!! Nimekumbuka wimbo huu ni wa siku nyingi sana.
 
Aliwasimanga sana madereva kwenye wimbo huu
Hakuwasimanga, alichofanya ni kutumia kipaji chake cha usanìi kutunga wimbo (siku hizi mnaita nyimbo) baada ya hotuba ya Nyerere.

Maneno yote kwenye wimbo yalikuwemo kwenye hotuba ya Nyerere.

Hotuba nzuri sana kuhusu utunzaji wa mali za umma unayoweza kuipata TBC ukiihitaji.
 
Asante sana
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…