Vituko vya maisha ya uswahilini

Hahaaahh na kuna wale wanaokaanga vitunguu swaumu ili mjue wanapika pilau
Vikishaungua na kutoa harufu kwa majirani basi jiko linazimwa na kama nichai anakunywa au kama hamna cha kuliwa basi anapiga desh. Teh.

Na mwisho wa siku maisha yanasonga.Ila sijajuaga nini inasababisha aisee.
 
Hahahhh.. Watu wana tabu
 
Uswahili pekee mademu huazimana nguo kwa ajili ya mtoko na wanajua balaa kupangilia pamba

Wana mapenzi ya dhati wanajua kupendeza unaweza jua huyu matawi ya juu akikupeleka sasa kwao utakimbia lakin kwenye kuvaa nawapa 100%
 
Daah...! kuna wale ambao akisikia tu kuna sauti ngeni nyumba ya pili atafanya juu chini awaone, mara utaona anakuja kuzima hata visivyo azimika ili mradi tu awone wagen wangu🙁
Ukipata majirani wa hivyo mshukuru Mungu, huku uswahilini kwetu ni mwendo wa kupiga chabo dirishani tu.
 
Uswahili pekee mademu huazimana nguo kwa ajili ya mtoko na wanajua balaa kupangilia pamba

Wana mapenzi ya dhati wanajua kupendeza unaweza jua huyu matawi ya juu akikupeleka sasa kwao utakimbia lakin kwenye kuvaa nawapa 100%
Wapo vizuri sana,mimi napendaga wakiwa wanajiandaa na shughuli ya mwenzao na yale madela yao ya saresare
 
Kuna Ndoa nyingine uswahilini utakuta ni mwaka wa kumi huu Mke haijui sura ya mumewe Mchana inafananaje,
Jamaa anatoka alfajiri saa 11 anamwacha wife kalala anarudi usiku saa 6 kila siku.

Haya maisha yafike mahali yatuonee huruma jamani[emoji3]
 
Mambo ya uswahilini kuvunja nazi njia panda,
Kufua kondomu ulizotumia na kuanika kwenye kamba uani!
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…