Vituko vya Mike Tyson

Hadithia na kile kisa cha kukamatwa kafungulia mziki mkubwa kwenye gari
 
The Boss siku hizi ana project za kulima bangi zinamuingizia pesa nyingi japo wadadisi wanasema baada ya kufilisika amejiunga pia na magenge ya wauza unga
 
Hawa jamaa wanasema net worth yake now ni 3 millio dollars

 
Mtu mzima Mike Iron Tyson.

Hapo kwenye Bentley nimecheka kinoma.
 

Tyson aliathirika kutokana na mazingira aliyokulia. Aliathirika zaidi Cus alipofariki, coz jamaa ndio alikuwa anamuongoza katika mengi.

Btw, the night aliyomuachia Ed Bentley, alinunua si chini ya chupa 20 za champagne. Ilipofika ngoma nane, akanunua bar yote. Hakuwa na nidhamu kabisa ya hela. Cha msingi amegundua alidondoka wapi na amebadilika.
 
Dah kweli jamaa ameanguka vikubwa.
Toka utajiri wa $ 300 millions mpk $ 3 millions!
Yani $ 297 millions zote pukupuku manyoyer!
Amezingua sana yeye na Diamond,Diamond ana hela kwa sasa.
Asee ila amejifunza kutokana na makosa.
 
Tyson kichaa, halafu very giving, to a fault. Inabidi awe na money manager anayempa money discipline all the time. Ama sivyo ataunguza hela.

Parties zake zilikuwa za vinywaji na vyakula vya bei mbaya, halafu wakati wa kuondoka kila mualikwa anapewa saa ya Rolex ya dhahabu ya bei mbaya

Ila uzuri ni kwamba anajua sana kuji reinvent, halafu Wamarekani wanampenda sana vituko vyake vyote wanamsamehe, kwa sababu anaonekana mtu real. Halafu Tyson ana side fulani ambayo iko very down to earth na cool.

Yani amekuwa more than just a boxer, sasa kaingia mpaka kwenye pop culture. Nilikuwa nasoma kitabu kimoja cha Lawrence Freedman kinaitwa "Strategy:A History". Kinaelezea history and evolution of strategic thinking, nukuu ya kwanza ya kitabu ni ya Mike Tyson alisema "Everyone has a plan, 'till they get punched in the mouth". Kimsingi alielezea namna gani mipango makini inaweza kusahauliwa ukipatwa na dhahama ya ghafla. Nikaona Tyson anaheshimiwa na wahuni wavuta bangi wa Brooklyn mpaka hawa respected New York Times/Ivy League bestselling authors. That is a rare combination.

Sasa hivi ana kampuni yake ya kuuza bangi, anasema wanavuta na kugawa kwa wafanyakazi wake bangi ya dola $40,000 kila mwezi.


Hizo clubs za Manhattan kama hauko on point katika mavazi wanakukatalia kuingia. Mimi enzi zangu za kwenda club walikuwa wanafikiri ni US Marine kwa sababu ya nywele nilivyonyoa halafu na kifua cha kupiga chuma.

Siku moja Webster Hall bouncer alikuwa anawapiga watu chini kichizi, kufika mimi akanifungulia njia anasema "thank you for your service" (msemo wa kuwashukuru wanajeshi wa Marekani ambao raia wengi husema).

Nikasema kwa leo nitakuwa mwanajeshi tu.
 

Alivyofilisika kuna jamaa alijitokeza kumsaidia ku recover
Ndie alikuwa behind hadi kipindi kile anatokea kwa Oprah na Holifield
na akawa na tv program Fox TV i guess kinaitwa 'being Mike Tyson'
aka recover hadi net worth ikawa inasoma 5 to 10 millions..
sijajua what happened lakini naona so far anaendelea vizuri...ni kweli Tyson
ana kitu fulani hivi special ambacho kinafanya awe na mvuto tofauti sana..
naona hiyo kuwa real na genuine.na life yake ndo siri pengine
 
Jamaa alinifurahisha sana siku moja alihojiwa, akaulizwa kitu gani anapenda kufanya?

Basi mwenyewe najua huyu Mike Tyson atataja kitu cha kuhusu mazoezi, uwezo wa kiriadha au kupigana, ubabe, silaha, magari ya kasi, na habari kama hizo.

Akajibu kwamba kitu anachopenda kabisa ni kufuga njiwa, kwamba tangu alivyokuwa mdogo alikuwa anafuga njiwa katika mabanda ya rooftop Brooklyn.

Nikasema "this is so "On The Waterfront".

Kama umeona hiyo movie utaona New Yorkers wa zamani walivyopenda kufuga njiwa. Tyson at heart is a loving person, na Wamarekani wengi wanaona hayo na wanamkubali.
 
Ukisikia chubwiii imezama hiyooo
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…