Follow along with the video below to see how to install our site as a web app on your home screen.
Note: This feature may not be available in some browsers.
Tyson now ana pesa kidogo
ame recover kiasi
Kuna jarida nilisoma last year wanasema $200M. Hazimpigi chenga sii haba, tunamsubiri myweather nae tuone
Ni muigizaji pia na ameingia ktk Chinese film industry.The Boss siku hizi ana project za kulima bangi zinamuingizia pesa nyingi japo wadadisi wanasema baada ya kufilisika amejiunga pia na magenge ya wauza unga
pesa nyingi na madawa vilimfanya awe kama chizi
sio sifa kuita vituko hasa kama hiko cha Bentley..ndo maana
Tyson hajui hadi leo alitumia vipi utajiri wa zaidi ya dolla milioni 300
akafilisika
ni hadithi za kusikitisha jinsi alivyozungukwa na 'wezi' waliojifanya washkaji
Siku mojaTyson alisimulia alikuwa akitaka watu waende kumfulia nguo
watu wanapigana nguo kugombea nguo zake wakafue
baadae ndo alikuja kugundua kumbe alikuwa anaacha pesa nyingi hadi dollar elfu 30
kwenye nguo ndo kilichofanya watu wapiganie nguo zake
alipofilisika wote wakamkimbia
Hawa jamaa wanasema net worth yake now ni 3 millio dollars
![]()
Mike Tyson Net Worth
What is Mike Tyson’s net worth? Introduction Mike Tyson is an American former professional boxer with an estimated net worth of . He had a successful 20-year career within the sport. Despite a few ups and downs along the way. Tyson was the undisputed world heavyweight champion and still holds...wealthygorilla.com
😂 😂 😂 😂 😂Mawazo yangu yote nilikuwa najua Tyson ni mtanzania. Yaani nimekuja kujua wakati wa balehe 2012 kuwa jamaa siyo mtanzania.
Tyson kichaa, halafu very giving, to a fault. Inabidi awe na money manager anayempa money discipline all the time. Ama sivyo ataunguza hela.pesa nyingi na madawa vilimfanya awe kama chizi
sio sifa kuita vituko hasa kama hiko cha Bentley..ndo maana
Tyson hajui hadi leo alitumia vipi utajiri wa zaidi ya dolla milioni 300
akafilisika
ni hadithi za kusikitisha jinsi alivyozungukwa na 'wezi' waliojifanya washkaji
Siku mojaTyson alisimulia alikuwa akitaka watu waende kumfulia nguo
watu wanapigana nguo kugombea nguo zake wakafue
baadae ndo alikuja kugundua kumbe alikuwa anaacha pesa nyingi hadi dollar elfu 30
kwenye nguo ndo kilichofanya watu wapiganie nguo zake
alipofilisika wote wakamkimbia
Tyson kichaa, halafu very giving, to a fault. Inabidi awe na maney manager anayempa money discipline all the time. Ama sivyo ataunguza hela.
Ila uzuri ni kwamba anajua sana kuji reinvent, halafu Wamarekani wanampenda sana vituko vyake vyote wanamsamehe, kwa sababu anaonekana mtu real. Halafu Tyson ana side fulani ambayo iko very down to earth na cool.
Yani amekuwa more than just a boxer, sasa kaingia mpaka kwenye pop culture. Nilikuwa nasoma kitabu kimoja cha Lawrence Freedman kinaitwa "Strategy:A History". Kinaelezea history and evolution of strategic thinking, nukuu ya kwanza ya kitabu ni ya Mike Tyson alisema "Everyone has a plan, 'till they get punched in the mouth". Kimsingi alielezea namna gani mipango makini inaweza kusahauliwa ukipatwa na dhahama ya ghafla. Nikaona Tyson anaheshimiwa na wahuni wavuta bangi wa Brooklyn mpaka hawa respected New York Times/Ivy League bestselling authors. That is a rare combination.
Sasa hivi ana kampuni yake ya kuuza bangi, anasema wanavuta na kugawa kwa wafanyakazi wake bangi ya dola $40,000 kila mwezi.
![]()
Mike Tyson has a marijuana farm and smokes $40,000 worth of weed a month
Tyson is selling $500,000 worth of marijuana to dispensaries each month.mashable.com
Hizo clubs za Manhattan kama hauko on point katika mavazi wanakukatalia kuingia. Mimi enzi zangu za kwenda club walikuwa wanafikiri ni US Marine kwa sababu ya nywele nilivyonyoa halafu na kifua cha kupiga chuma.
Siku moja Webster Hall bouncer alikuwa anawapiga watu chini kichizi, kufika mimi akanifungulia njia anasema "thank you for your service" (msemo wa kuwashukuru wanajeshi wa Marekani ambao raia wengi husema).
Nikasema kwa leo nitakuwa mwanajeshi tu.
Jamaa alinifurahisha sana siku moja alihojiwa, akaulizwa kitu gani anapenda kufanya?Alivyofilisika kuna jamaa alijitokeza kumsaidia ku recover
Ndie alikuwa behind hadi kipindi kile anatokea kwa Oprah na Holifield
na akawa na tv program Fox TV i guess kinaitwa 'being Mike Tyson'
aka recover hadi net worth ikawa inasoma 5 to 10 millions..
sijajua what happened lakini naona so far anaendelea vizuri...ni kweli Tyson
ana kitu fulani hivi special ambacho kinafanya awe na mvuto tofauti sana..
naona hiyo kuwa real na genuine.na life yake ndo siri pengine
Moja kati mabondia bora kabisa kuwahi kutokea. Binafsi huwa navutiwa sana na vituko vyake enzi hiyo. Vilivyonivutia sana ni hivi...
Kwa mujibu wa Fat Joe. Siku moja Joe na Big Pun walibananishwa nje ya club (The Tunnel) na bouncers kama 8 hivi wakitaka kuwachapa baada ya kurushiana maneno. Enzi hiyo Joe na Pun ni mijitu ya miraba 16, na walikuwa na uwezo wa kupambana, ila walikuwa heavily outnumbered na wale bouncers, na mijamaa iko 7ft huko, so ikabidi wawe wapole ila too late. Ghafla Iron Mike katokea, "wa'thup Joe and Pun! I got your back" (not quite sure that's what he said tho). Tyson akavua viatu, akaanza kuwakimbiza wale bouncers huku wakiwaomba kina Joe wawaombee msamaha kwa Tyson. Tunaongelea bouncers 8 wanamkimbia Mike. Joe na Pun walibaki kucheka na kushukuru miungu yao kwa kuepuka kipigo.
Story ya Ed Lover. Ed siku moja anaingia zake club moja, Manhattan. Akakutana na Mike anatoka nje. Mike akamuambia hiyo club hakuna issue, so wanaelekea club ingine in Queens, na Ed awafuate. Ed akaacha gari yake pale club, akaingia kwenye msafara wa Tyson. Kufika club, bouncer akawachomolea kuingia sababu kulikuwa na dress code. Ilibidi mmiliki aitwe, ndio wakaingia. Baada ya kula bata zito, muda wa kwenda home sasa Ed anamwambia Tyson ampe mtu amrudishe Manhattan alipoacha gari yake. Tyson akamwambia hapa wote tumechoka, akamuachia Bentley aliyokuwa anaendesha yeye, 450k worth. So Ed akaenda home kwa mama ake kulala, akitegemea Tyson atamcheki kesho yake ili arudishe gari. Wiki ikapita kimya, wiki ya 2, mpaka mwezi mzima ndio manager wa Tyson anamcheki Ed kumuuliza kama ana gari yoyote ya Mike. Ed akawapa address, wakaifuata gari. 15 years later, Ed anakutana na Tyson Las Vegas. Katika stori, Tyson anamwambia Ed kuwa ile Bentley alimuachia mazima, manager wake tu alipatwa na wivu ndio akamyang'anya.
Jamie Foxx's story. Wakati Jamie ndio anaanza ku-blow up, moja kati ya jokes zilizokuwa zinampa shangwe la kutosha ni ya kumuhusu Tyson. So siku moja anapiga show, watu wanakubali balaa, kufika kwa joke ya Mike...watu wote kimya, hakuna anayecheka. Kumbe mtu mzima yupo ukumbini mule, Jamie akaishiwa pozi kabisa. Long story short, Tyson alimwambia to tell the joke, but it better be funny.
Comedian Godfrey's. G siku moja yuko out and about, akakutana na Tyson akiwa dame ambaye jamaa anamjua. Yule dame akamsalimia mchizi, mchizi akamkana dame kuwa hamjui wala hajawahi kumuona maisha yake yote. Usifanye mchezo.
Ziko nyingi sana, ila hizo zilinivutia zaidi.