Vituko vya Mwananyamala: Mtaa kwa mtaa (special thread)

Yale maneno ndo raha ya draft yenyewe,unasikia jamaa anakuambia eti" Mimi nimewahi pewa mke na mimba yake sababu ya hivi vitu sasa wewe unakuja kujifunzia kwangu" hahahaha
Kuna mmoja alikuwa Tanga huwa anasema " Akishawai kuhamisha watu msikiti"
 
Nakumbuka mtaani kwetu kulikua na grocery mdada mmoja waki kipare auntie rosse ndio ilikua grocery yake wateja wake wakuu walikua matapeli wa kino, m'nyamala na na manjunju wakina nassoro mwenye sonara na yule tapeli maarufu wa manjunju anaitwa juma nani sijui halaf sasa hivi auntie rosse kaokoka asee kweli maisha yanabadirika
 
Naitwa mjushi naishi tandale..njoo jukwaa la tv kule tufanye kazi acha mbinu zako za mwijuma ktk makorokoro ulikuwa unakula mabumunda shunie hatari
[emoji23][emoji23][emoji23][emoji23][emoji23][emoji23] kwendraa zako nilikua napenda kachori za yule mama na supu na ndizi na nyama za yule mama mama muuza ndizi na zile ice cream kubwa za orange
 
Mabingwa wote wana kopi zao ukicheza tuu anajua hiyo kopi ni ya nani.
Kuna siku watu wamecheza kete mbili mbili tu wanapanga suluhu.

Kuna siku nilipita mabibo hostel pale kwa wauza viatu kuna Mzee mmoja alimfunga mwanachuo kisha akamuuliza wewe unasona Chuo?
jamaa akasema ndio. Mzee akamwambia " hufai kuwa chuo huna akili za draft huko chuo itakuwaje"
 
Dah mwananyamala duh kuna teja alikuwa kachoka akawa hana nguvu ya kukaba tena alikuwaga ana kaba roba za mbao madawa yaka mchosha alikuwa anaishi mwananyamala kwa KWAKIDILE baada ya kuchoshwa na madawa Akawa anavizia watu asubuhi anatoka na kapu lake na kanzu chafu kama vile kuna sehemu anawahi na kibakora ukimuona kama vile mzee wa miaka 60!!
Anatoka zake asubihi alifajiri kwenye kapu lake utaweza hisi anaenda sokoni au ana mpelekea mgojwa uji asubuhi kumbe kwenye kapu kuna mawe anavizia wale wanakwenda asubuhi sana kazini alfajiri akikutana na mtu yuko mwenyewe anampisha apite akipita tu anachomoa jiwe kwenye kapu lake alikuwa hakose anampiga lakichwa mtu anapoteza faham anamchukulia viatu pesa alikuwa hatumie dakika moja mtu anakuwa ameshachukuliwa vitu vyote!!!
mtu akishituka yupo hosipitali anasema nilikuwa mwenyewe nyuma yangu alikuwepo Babu mmoja alikuwa hawezi kutembea ata vizuri kwa Mnao kumbuka vizuri ilikuwa Enzi za kina MaGANGA!!

Duh MWANANYAMALA nimeishi adi mtu aje kuniibia au kuniingiza mjini duh sidhani kama itawezekana asante mwananyamala palinifundisha mengi !!

Mwananyamala nimewahi kukuta mateja yame mzunguka jamaa wanalilia viatu vyake kuwa jamaa kawaibia kwa wana mtaka avuwe awape
Kuna watu walikuwa wna vua unakuta jamaa wana sindano wana jidunga madawa na sindano inadamu kibao ila uzuri wa hao mateja wakiwa wana kujuwa unapita hawakufanyie chochote ila ukitaka kujuwa ubaya wao uwatibulie mitego yao
kwa wanaoishi Mwananyamala ya sasa nisawa na wanaoishi mbezi!!
 
Naitwa mjushi naishi tandale..njoo jukwaa la tv kule tufanye kazi acha mbinu zako za mwijuma ktk makorokoro ulikuwa unakula mabumunda shunie hatari
Nakucheck now wassap
 
Nimeondoka hapo kitambo sanaa hivi ule uwanja wa spurs bado upo ,aise pale ilipigwa mechi moja Kali miaka ya 2001 Kati ya faru dume ya manzese na timu nyingine nimeisahau aise ile mechi baada ya firimbi ya mwisho tu uwanja ukageuka kuwa wa vita.
FARU ya manzeseBEACH BOY ya ferry NATIONAL ya tandale hizo timu zikija kucheza na SWAZI lazima watu kbla mpira hujaisha tutokee kwenye mabati
 
Haha...inavyoonekana wanajamii Forum wengi wanaishi au wamewahi kuishi mwananyamala...manake mnavotiririka...hatar sana
Ukiwa umekulia dar watu Wa Mwananyamala lazima ukutane nao ktk mpira ndondo au ligi za mchangani , beach club au shuleni lazima waraouathiri tuu au utapata story zao au kuzushuhudia
 
Mshana umenikumbusha hali tete mwananyamala. Nina nyumba ndogo mkwajuni nilitembelea huko jamaa Waka mind mzigo Wangu wakataka wanifanyie kweli, nilichowafanyia mpaka leo wana historia yangu. na nyumba yangu ndogo mpaka leo wanaiheshimu. huwa wanamuuliza jamaa yako ni nani? anawaambia kamuulizeni mwenyewe.
 
Bila kumsahau mtuma salamu maarufu na mshiriki wa kipindi cha chemsha bongo...Mohamed Kiyaiyai..mzee wa niambrieeeee...kutoka KomaKoma .
Huyu alikuwa anazinguana sana na Misanya Bingi...yaani akipiga simu anaanza kutaja washikaji walioko pembeni yake kama kumi hivi halafu ndio aanze kuwatumia salamu watu watatu...yaani ndani ya sekunde 60 anakuwa keshatuma salamu kwa watu zaidi ya 15 hivi....Misanya Bingi alimshtukia akawa anamgongea kipusa na kumkata hewani.
Halafu misanya alikuwa anamkomesha kwa kugonga kipusa kama dakika moja hivi...yaani ukitafsiri ni kama vile alikuwa anamporomoshea mitusi kwake na kwa ndugu na masela wake.

Yaani huu utundu wa wabongo ungekuwa ni wa kutengeneza vyombo vya anga mwezini tungekuwa tushahamia.
 
Nimemshangaa sana huyo jamaa...hivi anadhani tukikutana kama wanaJF basi kutatokea ngumi ...by the way ni muhimu watu wakatambua tu watanzania na wote tunaitakia mema nchi japo kwa approach tofauti.
Kwenye uzi huu kuna reflection kubwa ya maisha yetu kama wabongo !
 
[emoji1] [emoji1] [emoji1] [emoji1] Watu wa draft wana shombo sana
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…