Vituko vya Mwananyamala: Mtaa kwa mtaa (special thread)

Hili ni ziwa ambalo lipo miaka nenda rudi uko Mwananyamala, lakini kwa kipindi iki cha mvua na mafuriko, watu wengi wanafikiria kuwa ziwa ili limesababishwa na haya mafuriko yanayotokea hivi sasa jijini Dar es salaam Kiasi cha wengi kufikiria kuwa satellite za google zimejichanganya na kuona kuwa kuna ziwa...

Ukweli ni kwamba ili ziwa lipo na halikusababishwa na mvua au mafuriko yanayotokea hivi sasa.

Lake Mwananyamala linatenganisha baina Mwananyamala na Kijitonyama au Tandale kwa Alimauwa.
 
Huu Uzi umenichekesha sana nimesoma Mwanzo mwisho japo ni WA zamani sana @mshanajr Mimi sijawahi kukaa mwananyamala ila niliwahi kukaa kinondoni shamba napo kwa muda mfupi unamjua haji mkambi? Alikua mwizi balaa ingawa alishafariki yeye na wenzake wa walipigwa tukio viwanja vya Biafra na wananchi wenye hasira Kali it was around 2008 au 2009.

nasikia matukio yao walikua wanapiga nyamala enzi hizo? Aliwahi nikosa kosa Alafu nilikua mwanafunzi maskini bahati nzuri walitokea watu wananijua na wanamjua wakamwambia haji huyu mdogo etu ole wako, iwe Mwanzo na mwisho na uwaambie wenzio wote asiguswe huyu😃😃😃😃
 
Msisiri B Shule ya msingi pale ndipo panaitwa "mbuzi kagoma kwenda" wanawake wanachota maji, anavutwa darasani anapigwa chuma mchicha ndani ya dakika 5 anarudi kwa mumewe na haitakaa ifahamike, hufanyika nyakati za jioni.
Kweli unapafahamu..[emoji23]
 
Mkongwe
 
Uzi umefufuka.. Nakumbuka mengi mengine nayasahau halafu nayakumbuka tena
 
Hahahhaa!!tulihama kitambo ila lile life la Nyamala silisahau kulikua na mpemba muuza duka pale ujiji aliibiwaga miaka ya 90 mwishoni na akakatwakatwa mapanga nusu afe,basi akapelekwa Hosp akatibiwa akapona alivyopona wale wezi walikufaa woteee!mmoja wa mwisho alikua jirani yetu alikua anaitwa Mussa alichomwa moto mapinduzi pale sokoni

Sent from my Infinix X559C using JamiiForums mobile app
 
Yako mengi ya kuandika kuhusu Mwananyamala siwezi kuyamaliza yote... Mengine yataandikwa na kusimuliwa na WanaJF - Mwananyamala Wing...[emoji23]
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…