Mada ya James Ngomero bingwa mtuhumiwa wa vichanga 11 imenikutanisha na watu wengi ambao kwa namna moja ama nyingine tunaweza kuwa tunafahamiana kabisa...
Si hilo tu bali nimegundua sehemu kubwmateja ana JF Dar wing ni wakazi wa Mwananyamala/ Kinondoni katika ujumla wake... Kuishi Mwananyamala pekee ni chuo tosha... Ikiwapendeza kwa uwingi wetu tunaweza kuwa na huu uzi wa vituko vya Mwananyamala mtaa kwa mtaa... Naamini kama umeishi Mwananyamala hutokosa cha kusimulia
1. Madawa ya kulevya ; Mwananyamala eneo lote la Mwananyamala A ni kituo na kitovu kikubwa cha madawa ya kulevya kuanzia wauzaji mapusha mpaka watumiaji... Hospital ya mwananyamala ina kituo cha kutoa tiba kwa mateja na nadhani ndio kituo kikubwa zaidi Tanzania
2. Hospital ya mwananyamala ; ndio hospital maarufu zaidi yenye vituko na kashfa nyingi... Kuanzia kutoa mimba, kashfa ya vichanga 11, wizi wa maiti, rushwa... Maiti iliyofumuliwa na kutolewa madawa na madaktari kuiba hayo madawa,... Nknk
3. Matapeli ; hapo ndio kwake.. Mitaa maarufu ikiwa ni kuanzia kwa Kopa, A mpaka karibu na Kinondoni B, wale matapeli maarufu mmoja akijulikana kama doctor... Wale matapeli kiboko wa Jerry muro bar yao kubwa ilikuwa nyuma ya hospital ya mwananyamala
4. Ofisi na kampuni za mifukoni.. Eneo lote la Kinondoni mkwajuni mpaka biafra ni hatari kwa shughuli hizo.. Utataka nini ukose.. Mihuri ya siri? Nyaraka za serikali? Mikataba mbalimbali, nyaraka za kusafisha mizigo.. Pesa bandia, madini bandia.. Kila kitu hukosi hapo
Mitaa hiyo ni maarufu kwa madaktari feki, wanausalama, polisi, wanajeshi mahakimu wanasheria, wabunge hata mawaziri nk
5. Machangudoa wasagaji mashoga Mario nk... Mtaa wa wibu ndio kama kitovu cha mashoga.. Ukiwasikia kina anti abuu, anti Ali hiyo ndio ilikuwa mitaa yao.. Habari za Machangudoa na wasagaji zinajulikana wazi.. Kinondoni na Mwananyamala ndio headquarters
6. Wezi, vibaka majambazi, wakora nao wako.. Ukisikia roba za mbao na watu wanaitwa mbavu Mwananyamala ndio kwao
7. Wachawi wanga na waganga... Wamo pia.. Mwananyamala kuna military base kubwa sana/KILINGE ya wachawi.... Lile anga limechafuka
8. Wasanii wanamuziki wa aina zote bongo movies, taarab, nk kaliba yote hii kwa sehemu kubwa chimbuko ni Mwananyamala
9. Wahamiaji haramu, wakongo wamalawi wakenya waganda warundi nk... Sehemu kubwa wamejazana Mwananyamala
Yako mengi ya kuandika kuhusu Mwananyamala siwezi kuyamaliza yote... Mengine yataandikwa na kusimuliwa na wana JF, Mwananyamala wing...