Mpaka sasa hivi sijaona sehemu zimetajwa bei za simu.
Sijawahi kununua simu dukani.
Simu yangu ya kwanza ya gharama kabisa kununua ni G Tide nilinunua 40,000 kwa Inno.
Ya pili 50,000 ilikua ndiyo enzi za simu za kichina kubwa kama kiganja.
Ya tatu 40,000 nokia 6300.
Siku hizi simu za range kama Samsung Galaxy s4, A3, J7, Note 2,3, LG G1,G2, G3, HTC one M8, one m9, Huawei p7, 8, 9, Y5, Y6 ni 150 au chini na haizidi 200, ukinunua zaidi ya hapo tunakucheka. S5, Note 4, 5, ni 200 mwisho 250.
Simu ambazo hazina soko ni Nokia Lumia na Blackberry, BlackBerry Torch mwaka 2013 ilikua bila 300 hujainyanyua siku hizi 40,000 sijaona ikizidi 60,000.
Iphone 5 iwe C au S haizidi 200, 6 iwe plus au nini unakula kuanzia 200 haitazidi 300. Iphone 7 kupanda sizioni kabisa.
Itel sisemi.
Nilikuta humu mtu anauza Tecno C5 200k nikamwambia yesu atarudi atakukuta nayo, huku hiyo ni 40,000 mpaka 100,000 kutegemea na muonekano wake. C8, J8, C9 ni range ya 130 mpaka 150.
Tecno H6, J7, zinaanzia 40,000 haizidi 80,000. Y3, y4, 30,000.
Huawei 530 na 500 ni 40,000
aisee hadi nachoka.
Kipindi kile ilikua ukipost tu humu inakuja ile 'Sent by simu hiyo hiyo using jamiiforums mobile app' mi nilikua naangalia baadhi ya majibu ya kifedhuli ya watu halafu naangalia na thamani ya simu yake.
Hawafanani