Vituko vya Mwananyamala: Mtaa kwa mtaa (special thread)

Vituko vya Mwananyamala: Mtaa kwa mtaa (special thread)

Kwa Dar M/nyamala ndio sehemu ambayo nilitokea kuigopa na nilikua napita mitaa yake kwa tahadhari kubwa,asubuhi mateja ni wengi maana wanakuja kuchukua dawa pale hospital,ukipishana nao inabidi uwe na makini unaweza porwa muda wowote...pale kwa Wahaya nilikwenda na jamaa yangu siku moja saa 6 usiku,walipotuona wakakimbilia ndani wakijua maaskari(mwanzo na mwisho wameweka wamasai wanalinda)kuna ufuska mkubwa unafanyika kwenye vile vijumba.

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Mpaka sasa hivi sijaona sehemu zimetajwa bei za simu.

Sijawahi kununua simu dukani.

Simu yangu ya kwanza ya gharama kabisa kununua ni G Tide nilinunua 40,000 kwa Inno.

Ya pili 50,000 ilikua ndiyo enzi za simu za kichina kubwa kama kiganja.

Ya tatu 40,000 nokia 6300.

Siku hizi simu za range kama Samsung Galaxy s4, A3, J7, Note 2,3, LG G1,G2, G3, HTC one M8, one m9, Huawei p7, 8, 9, Y5, Y6 ni 150 au chini na haizidi 200, ukinunua zaidi ya hapo tunakucheka. S5, Note 4, 5, ni 200 mwisho 250.

Simu ambazo hazina soko ni Nokia Lumia na Blackberry, BlackBerry Torch mwaka 2013 ilikua bila 300 hujainyanyua siku hizi 40,000 sijaona ikizidi 60,000.

Iphone 5 iwe C au S haizidi 200, 6 iwe plus au nini unakula kuanzia 200 haitazidi 300. Iphone 7 kupanda sizioni kabisa.

Itel sisemi.

Nilikuta humu mtu anauza Tecno C5 200k nikamwambia yesu atarudi atakukuta nayo, huku hiyo ni 40,000 mpaka 100,000 kutegemea na muonekano wake. C8, J8, C9 ni range ya 130 mpaka 150.

Tecno H6, J7, zinaanzia 40,000 haizidi 80,000. Y3, y4, 30,000.

Huawei 530 na 500 ni 40,000

aisee hadi nachoka.

Kipindi kile ilikua ukipost tu humu inakuja ile 'Sent by simu hiyo hiyo using jamiiforums mobile app' mi nilikua naangalia baadhi ya majibu ya kifedhuli ya watu halafu naangalia na thamani ya simu yake.

Hawafanani
Mkuu hapo kwa Inno Kuna boss wake Don wakuitwa chale mamba.yanii eneo la big M ndio ilikuwa Aggry ya mwananyamala simu ya aina yoyote unaipata kwa Inno na chale mamba hapo Big M(Aggry)
Fundi wao wa simu alikuwa pale LBC simu zote zinazoibiwa mwenge, makumbusho stendi zinapelekwa hapo LBC ndio zilikuwa zinabadilishwa IMEI No inaitwa kusilimishwa or kubadilishwa Dini
Yanii wew uwe mfanyakzi wa TCRA kabisaa simu yako ikishafika hapo kwa LBC aionekani Tena ktk system inabadilishwa Dini..
Mwananyamala hio

Sent using Jamii Forums mobile app
 
mwanyamala kiboko kuna jamaa tulimaliza nae form six alikuwa anishi mwananyamala tumemaliza pepa kama leo kesho wakanda coco beach na marafiki zake wa mwanyamala wakamumaliza huko huko
Mkuu huyu kijana unayemzungumzia hapa ni Elisha samwa?? Alikuwa Azania sec?
Kama ni kifo Cha Elisha samwa kijana ameondoka ktk hii dunia kwa kifo Cha utata Sana.
Alipotea tu gafra kila sehem ajaulikani alipo washikaji na wazee wake wakimuulizia.Baada ya siku tatu ikatambulika maiti yake imeonekana chumba Cha maiti ktk hospital ya mwanyamala na mtu aliyeitambua hio maiti ndio aliyezidisha utata Sasa ni bwana James ngomero (kitendo Cha ngomero yeye kuwa mtu wa kwanza kuiona or kutoa taarifa za kifo Cha Elisha kilizidisha mshangao ktk jamii kutokana na historia ya huyu ngomero)
Ilisemekana ameokotwa pwani ya Coco Beach akiwa mtu mfu
Pia kifo Cha Elisha kilihusishwa na imani za kishirikina (kitendo Cha mama mzazi kwende peke yake hospital ya mwananyamla na kuibeba maiti na kupotea nayo kawe ktk viwanja vya gwajima kipindi icho, na kitendo Cha mama kukataza watu kukusanyika na kulia msiba pale kwake)
Mpka Leo Elisha anakumbukwa Sana na vijana maana alikuwa genius wa mtaa alikuwa anajua vitu vingi Sana na shule alikuwa yupo vizur Sana japo na yeye alikuwa mpiga chabo mzuri Sana alikuwa anafika mpaka mkwajuni toka mwanayamala dirisha kwa dirisha kula chabo

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Mada ya Mfahamu James Ngomero: Bingwa mtuhumiwa wa zile maiti 11 za watoto hospitali ya Mwananyamala imenikutanisha na watu wengi ambao kwa namna moja ama nyingine tunaweza kuwa tunafahamiana kabisa...

Si hilo tu bali nimegundua sehemu kubwa wanaJF Dar wengi ni wakazi wa Mwananyamala/Kinondoni katika ujumla wake...

Kuishi Mwananyamala pekee ni chuo tosha... Ikiwapendeza kwa uwingi wetu tunaweza kuwa na huu uzi wa vituko vya Mwananyamala mtaa kwa mtaa... Naamini kama umeishi Mwananyamala hutokosa cha kusimulia.

1. Madawa ya kulevya: Mwananyamala eneo lote la Mwananyamala A ni kituo na kitovu kikubwa cha madawa ya kulevya kuanzia wauzaji mapusha mpaka watumiaji... Hospital ya mwananyamala ina kituo cha kutoa tiba kwa mateja na nadhani ndio kituo kikubwa zaidi Tanzania.

2. Hospital ya mwananyamala: Ndio hospital maarufu zaidi yenye vituko na kashfa nyingi... Kuanzia kutoa mimba, kashfa ya vichanga 11, wizi wa maiti, rushwa... Maiti iliyofumuliwa na kutolewa madawa na madaktari kuiba hayo madawa,... Nk nk.

3. Matapeli: Hapo ndio kwake.. Mitaa maarufu ikiwa ni kuanzia kwa Kopa, A mpaka karibu na Kinondoni B, wale matapeli maarufu mmoja akijulikana kama doctor... Wale matapeli kiboko wa Jerry Muro, bar yao kubwa ilikuwa nyuma ya hospital ya Mwananyamala.

4. Ofisi na kampuni za mifukoni: Eneo lote la Kinondoni Mkwajuni mpaka Biafra ni hatari kwa shughuli hizo.. Utataka nini ukose.. Mihuri ya siri? Nyaraka za serikali? Mikataba mbalimbali, nyaraka za kusafisha mizigo.. Pesa bandia, madini bandia.. Kila kitu hukosi hapo. Mitaa hiyo ni maarufu kwa madaktari feki, Wanausalama, polisi, wanajeshi mahakimu, wanasheria, wabunge hata mawaziri nk

5. Machangudoa, wasagaji, mashoga, Mario nk... Mtaa wa wibu ndio kama kitovu cha mashoga.. Ukiwasikia kina anti abuu, anti Ali hiyo ndio ilikuwa mitaa yao.. Habari za Machangudoa na wasagaji zinajulikana wazi.. Kinondoni na Mwananyamala ndio headquarters..

6. Wezi, vibaka majambazi, wakora nao wako: Ukisikia roba za mbao na watu wanaitwa mbavu Mwananyamala ndio kwao

7. Wachawi wanga na waganga Wamo pia.. Mwananyamala kuna military base kubwa sana/KILINGE ya wachawi.... Lile anga limechafuka.

8. Wasanii wanamuziki wa aina zote: Bongo movies, Taarab, na kadhali kaliba yote hii kwa sehemu kubwa chimbuko ni Mwananyamala

9. Wahamiaji haramu: Wakongo, Wamalawi, Wakenya, Waganda, Warundi nk... Sehemu kubwa wamejazana Mwananyamala.

Yako mengi ya kuandika kuhusu Mwananyamala siwezi kuyamaliza yote... Mengine yataandikwa na kusimuliwa na WanaJF - Mwananyamala Wing...
Mw/nyamala naijua toka miaka ya 90 nilikuwa naishi mtaa fulan nimeusahau jina(nyuma ya hospital ya mw/nyamala) karibu na kanisa fulan kubwa. Japo nilikuwa mdogo enzi hizo ila nlikuwa kati ya wababe wachache waliotawala mitaa hiyo. Nlikuwa under 10 yrs, lkn alikuwa akija dogo wa miaka 10, 11, hadi 12 namkalisha, Pia pamoj na udogo wng ila nilikuwa na uwezo wa kuruka gate la kanisa na kwenda kuiba vitu mbali mbali vilivyokuwa vikihifadhi hapo kanisani. Ila za mwizi 40 siku 1 mida ya saa 1 usk nlijikuta nimeingia kweny 18 ya mmakonde fulan ambae ndo alikuwa mlinzi wao hapo kanisan, waliponikamata yey na mama fulan wa kizungu ambae alikuwa anafanya kaz na masista wa kanisa hilo wakanipeleka hadi kwa uncle wang ambae muda huo ndio alikuwa akinilea. Aisee siku hiyo nilichezea kichapo ambacho mpaka leo sijakisahau. Pia kuna siku nilidandia gari watu wakaanza kupiga kelele "wee dogo shuka utakuja kufa" basi driver alivyosikia vile hakujua kinachoendelea akapata mshituko na kupiga break ghafla na akawa kama anarudi nyuma taratibu bila kujua nyuma kuna nani/nini wakati huo mimi nilikuwa nimeanguka basi wakati gari inarudi nikalala chali nimejinyoosha hapo ndo ikawa nusra yang. Toka siku hiyo uncle akaogopa kuendelea kuishi na mimi ikabidi anirudishe kwetu MB(mburahati) Dah aisee utoto raha hasa kwa sisi wa zawa wa mkoa wa Dar tumefaidi mamb mengi bingwa wng
 
Wale wenyeji wa mwananyamla Kuna kijana wenu wakuitwa Jumbe hivi Sasa amesharudi mtaani.kijana Jumbe alikuwa segerea toka 2015 masikani yake ilikuwa pale Torabora,jerusa na magomeni makuti

Kisa Cha kijana Jumbe kuwepo segerea akiwa na umri mdogo kabisa ni nyumba ya urithi..Hio nyumba ni urithi wa mama Jumbe alishafariki amebaki Kaka mtu yanii mjomba wa Jumbe hio nyumba ilikuwa na vyumba na wapangaji kadha wa kadha mjomba anapokea Kodi na kumpa chochote kitu kijana Jumbe Ina maana mama Jumbe alipofariki mjomba na Jumbe ndio waliobaki warithi pekee wa ile nyumba
Sasa huyu mjomba ni mtu kunusanusa unga(mteja) ilifika kipindi Jumbe apewi kabisa pesa za kodi na mjomba ukumbuke Jumbe nae ni chimbuko na damu ya mwanayamala bangi bangi
Basi bwana siku mmoja mchana wa jua Kali kabisaa Yule Jumbe akaenda kujipa dozi ya sawa sawa madawa,mapombe,bangi,maugoro mpka kichwa kikawaka sawa sawa akatafuta kibiriti na mafuta aina ya petrol liter kadhaa akiendea nyumba ya urithi akitia mafua yote wapangaji wapo, majirani wapo kijana alikuwa na bonge ya panga ukisogea karibu yake halali yake kijana Yule akaichoma ile nyumba mchana wa jua Kali kabisaaa
Nyumba ikawa inateketea kwa Moto kila mtu anaona na yeye amelisimamia zoezi vizur na panga lake mkononi yanii asisoge mtu kujaribu kuzima ule Moto mkubwa
Vijana kwa wazee,majirni,wapangaji wakabaki na mshango mkubwa huku watoto wadogo chini ya miaka mitano wakiimba(baadaya kuona gari ya kuzima Moto imekuja na vingora vinalia)watoto wakawa wanaimba "mjomba Jumbe kaleta fire fire fire" "mjomba Jumbe kaleta fire fire fire" uku Jumbe mwenye anacheza kwa mtindo wa mchiriku

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Mwenyekiti wetu hajui kusoma na kuandika ukaanzishwa utata akasema anajua kuandika na kusoma.

Wakakutanishwa siku hiyo ya kumtest kama kweli anajua kusoma na kuandika akaambiwa andika Chama Cha Mapinduzi.

Akaandika Chama Ha Mapundusi

Mwandiko kama bata.

Kampeni za 2015 akawa ananadi sera nanukuu

"Vijana nipeni kura mimi na nyinyi hatuna ugomvi ndiyo maana mnapovuta bangi napajua ila sijawahi kuwaleta polisi, kama kuna yeyote kawahi kusumbuliwa na askari kisa bangi aseme"
Hahahahaaaaaaaaa
 
Wale wenyeji wa mwananyamla Kuna kijana wenu wakuitwa Jumbe hivi Sasa amesharudi mtaani.kijana Jumbe alikuwa segerea toka 2015 masikani yake ilikuwa pale Torabora,jerusa na magomeni makuti

Kisa Cha kijana Jumbe kuwepo segerea akiwa na umri mdogo kabisa ni nyumba ya urithi..Hio nyumba ni urithi wa mama Jumbe alishafariki amebaki Kaka mtu yanii mjomba wa Jumbe hio nyumba ilikuwa na vyumba na wapangani kadha wa kadha mjomba anapokea Kodi na kumpa chochote kitu kijana Jumbe Ina maana mama Jumbe alipofariki mjomba na Jumbe ndio waliobaki warithi pekee wa ile nyumba
Sasa huyu mjomba ni mtu kunusanusa unga(mteja) ilifika kipindi Jumbe apewi kabisa pesa za kodi na mjomba ukumbuke Jumbe nae ni chimbuko na damu ya mwanayamala bangi bangi
Basi bwana siku mmoja mchana wa jua Kali kabisaa Yule Jumbe akaenda kujipa dozi ya sawa sawa madawa,mapombe,bangi,maugoro mpka kichwa kikawaka sawa sawa akatafuta kibiriti na mafuta aina ya petrol liter kadhaa akiendea nyumba ya urithi akitia mafua yote wapangaji wapo, majirani wapo kijana alikuwa na bonge ya panga ukisogea karibu yake halali yake kijana Yule akaichoma ile nyumba mchana wa jua Kali kabisaaa
Nyumba ikawa inateketea kwa Moto kila mtu anaona na yeye amelisimamia zoezi vizur na panga lake mkononi yanii asisoge mtu kujaribu kuzima ule Moto mkubwa
Vijana kwa wazee,majirni,wapangaji wakabaki na mshango mkubwa huku watoto wadogo chini ya miaka mitano wakiimba(baadaya kuona gari ya kuzima Moto imekuja na vigora vinalia)watoto wakawa wanaimba "mjomba Jumbe kaleta fire fire fire" "mjomba Jumbe kaleta fire fire fire" uku Jumbe mwenye anacheza kwa mtindo wa mchiriku

Sent using Jamii Forums mobile app
[emoji44][emoji44][emoji44][emoji44][emoji30][emoji30][emoji30][emoji848][emoji848][emoji848][emoji23][emoji23][emoji23][emoji23][emoji23][emoji23][emoji23][emoji23][emoji23][emoji23][emoji23][emoji23][emoji23]duu kwahiyo akahukumiwa kwenda lupango?

Jr[emoji769]
 
Mw/nyamala naijua toka miaka ya 90 nilikuwa naishi mtaa fulan nimeusahau jina(nyuma ya hospital ya mw/nyamala) karibu na kanisa fulan kubwa. Japo nilikuwa mdogo enzi hizo ila nlikuwa kati ya wababe wachache waliotawala mitaa hiyo. Nlikuwa under 10 yrs, lkn alikuwa akija dogo wa miaka 10, 11, hadi 12 namkalisha, Pia pamoj na udogo wng ila nilikuwa na uwezo wa kuruka gate la kanisa na kwenda kuiba vitu mbali mbali vilivyokuwa vikihifadhi hapo kanisani. Ila za mwizi 40 siku 1 mida ya saa 1 usk nlijikuta nimeingia kweny 18 ya mmakonde fulan ambae ndo alikuwa mlinzi wao hapo kanisan, waliponikamata yey na mama fulan wa kizungu ambae alikuwa anafanya kaz na masista wa kanisa hilo wakanipeleka hadi kwa uncle wang ambae muda huo ndio alikuwa akinilea. Aisee siku hiyo nilichezea kichapo ambacho mpaka leo sijakisahau. Pia kuna siku nilidandia gari watu wakaanza kupiga kelele "wee dogo shuka utakuja kufa" basi driver alivyosikia vile hakujua kinachoendelea akapata mshituko na kupiga break ghafla na akawa kama anarudi nyuma taratibu bila kujua nyuma kuna nani/nini wakati huo mimi nilikuwa nimeanguka basi wakati gari inarudi nikalala chali nimejinyoosha hapo ndo ikawa nusra yang. Toka siku hiyo uncle akaogopa kuendelea kuishi na mimi ikabidi anirudishe kwetu MB(mburahati) Dah aisee utoto raha hasa kwa sisi wa zawa wa mkoa wa Dar tumefaidi mamb mengi bingwa wng
[emoji23][emoji23][emoji23][emoji23][emoji23][emoji23][emoji23][emoji23][emoji23][emoji23]kurudi MB ndio yakawa yale ya komando yosso?

Jr[emoji769]
 
[emoji44][emoji44][emoji44][emoji44][emoji30][emoji30][emoji30][emoji848][emoji848][emoji848][emoji23][emoji23][emoji23][emoji23][emoji23][emoji23][emoji23][emoji23][emoji23][emoji23][emoji23][emoji23][emoji23]duu kwahiyo akahukumiwa kwenda lupango?

Jr[emoji769]
Amesota Sana segerea ila sijui imekuaje ajapata hukumu ila miaka mingi alikuwa segerea kwenda mahakaman na Kurudi...now yupo mtaani wanauza Lile eneo Kama plot Sasa

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Back
Top Bottom