Ni kosa kubwa kumwachisha kazi mkeo kwa sababu: 1. sheria ya ndoa inakutaka wewe kuangalia familia - isome tafadhari; 2. ukimwachisha kazi hayo mahitaji yake binafsi utayagharamia wewe upende usipende kwani keshazoea huyo, ukigoma tu wanaume wenzako watagharimia; 3. ukifa au ukifukuzwa kazi yeye lazima atasaidia tu; 4. kunawatanzania wengi wanahudumiwa naye hivyo ni kuwanyima haki; 5.
kusoma kwake ni investment ambayo sasa inazalisha - faida kitaifa na kibinafsi. Je, watoto wakimuomba kitu anawanyima au anawaambia mwambieni baba? Hivi yale masufuria, masahani, vijiko jikoni unanunua wewe tu? Sasa angalia humo ndani kwenu je vyote umenunua wewe? Nyumbani kwao unapeleka misaada kama wanahitaji au yeye tu? Je, wewe upeleki pesa kwingine bila yeye kujua? Je, wewe sio mtu wa mitungi? Raha ya mwanaume wa shoka ni kuhudumia familia kwa kila kitu! Labda kwenye kitchen party aliambiwa kazi yake ni moja tu kulea na kukupa wewe penzi moto moto!!!