Mkuu hapo utakuwa umekosea mwenyewe awali. Hawa viumbe imeandikwa "muishi nao kwa akili". Ukikosea step tu na akakutune kama mitabendi ya radio, utapiga muziki kila kukicha na asicheze...Kama uliamua kuanza na kujibebesha jukumu la kumwachia mshahara wako aupangie matumizi, ni waz kuwa wakwake utapumzika kwa mambo yake. Japo ndoa ni wawili lakini inapokuja kwenye masuala ya vipato, wanandoa wengi wanakosa kushirikishana, mwengi ya kina mama hela zao zinahishia zaidi kwanye matumizi binafsi hasa "kujikwatua" au kusaidia kwa upande wa alikotoka (weyewe wanaita kwetu). Wakati huo huo akina baba huwa hela zao ukiacha matumizi ya nyumbani kama chakula na matunzo ya familia, nyingi huwa zinaishia kwenye "kinywaji" (kwa wale wanaokunywa).
Ikiwa hamjakaa na kupoanga vizuri nini mfanye katika maisha, ni ngumu sana kuwezana inapofika kwenye suala la matumizi la matunda ya jasho la kila mmoja wenu. Kuna wakati inafikia kukosa pia kuaminiana na kufichana vipato ikiwa mwenzako unaona anatumia zaidi kwenye maene yasiyo na tija. Wengi wa wanandoa huwa hawaambiani hata marupurupu wanayopata kwenye kazi zao ukiacha mshahara.
Ukiwa katika mazingira kama hayo ambapo mama hataki kutumia kipato chake kwa ajili ya familia kwa kuwa baba upo na wewe ndio kichwa cha nyumba, hapo maisha ni sawa na kuishi na hawara/ kimada ndani ya nyumba ambae hamuaminiani wala kuonena huruma kwa kusaidiana. Katika maisha ya jinsi hiyo, ni nadra kukuta kuna maendeleo ya dhati. Mkeo akizoea kutumia kipato chake kwa manufaa yake binafsi, ni dhairi kuwa inamjengea ulemavu wa kujua majukumu. Ikitokea bahati mbaya ukifa, hata kama ana kazi itamwia vigumu sana kumudu majukumu ya familia kwa kuwa ana kuwa amezoea kuishi kwa kipato cha mume zaidi. Ndio haina ile ya wanawake ambao mume akifa inakuwa kama amepoteza muelekezo kabisa hata kama ana kazi nzuri, inachukua muda mfupi sana utamkuta kishapata Bwana mwingine.
Mkae chini mpange kwa pamoja, acha kuficha zako kwenye makoti au kabatini nae mweleze hivyo hivyo kuwa majukumu ya ndoa ni yenu wote (kwa shida na raha, magonjwa na huzuni).
Kumwachisha kazi haina suluhu, kwani itakuongezea mzigo tena hata hivyo vipodozi vyake itahamia kwenye hako kamshahara kako na pengine hata zile chache alizokuwa akimudu kutuma kwa wazazi wa upande wake (kama wapo na wanawategemea) zinapaswa zipukuchuliwe katika hako" ka salari" kako. Tena pengine si busara iwapo Mkeo amesoma kwa gharama za wazazi wake harafu wewe ushindwe kumsaidia kupata kazi au kumzuia hasifanye kazi, inakuwa kama vile umewadharau wale waliomsomesha mpaka alipofikia nawe ukamwona.