Vituko vya watoto juu ya misosi mbele ya wageni vinavyoaibisha wazazi!!

Vituko vya watoto juu ya misosi mbele ya wageni vinavyoaibisha wazazi!!

Ubumuntu

JF-Expert Member
Joined
Oct 21, 2010
Posts
14,387
Reaction score
10,965
Salaam,

Najua wote tunavyo (katika kumbukumbu) visa na vituko mbalimbali ambavyo wadogo zetu, watoto wa ndugu na marafiki na watoto zetu wameshawahi kuvifanya linapokuja suala la chakula. Vituko hivyo mara nyingi usababisha aibu na fedheha kwa wazazi ama walezi.

Mimi ninavyo kadhaa:

1. Kuna mtoto wa ndugu yangu siku moja alimwaibisha mama yake juu ya soda ya mgeni. Mambo yalikuwa hivi: mgeni alifika na kukaribishwa, baada ya muda bila kuona mgeni anahudumiwa na kinywaji, mtoto akauliza, "mama mbona haumpi mgeni soda"? Basi mama kwa kujibalaguza akajifanya alisahau na kuleta soda. Balaa likawa baada ya mgeni kupewa soda na kuanza kunywa, kwani mtoto alisema, "yaani pamoja na kukuombea soda kwa mama, hata kidogo hunipi"?
Mama na mgeni walibaki wameduwaa; kwani mtoto mwenyewe ni mwenye miaka 3.5 tu!!

2. Kuna mtoto wa jamaa yangu (jamaa uwa anajifanya mambo safi). Sasa siku moja mimi na jamaa zangu tulienda kumtembelea nyumbani kwake. Kama kawaida ya waafrika, ugeni upokelewa kwa mahanjumati ya kumwaga. Sasa ilipofika wakati wa msosi, mtoto wake wa kike (miaka 4) akaanza kama kuimba kila mara, "baba leo tunakula nyama, leo tunakula nyama, nyama nyingi sana, nyama nyingi sana"!!!
Mimi nilibaki nikuduwaa tu, maana sikutaraji hiyo hali.


Fundisho:

Fanya ufanyalo katika kuhangaika ili uweze kumfanya mwanao aone chakula siyo 'ishu'. Akiona msosi ni ishu, hakika atakuja kukuaibisha mbele za watu.
 
Back
Top Bottom