Wang Shu
JF-Expert Member
- Feb 1, 2014
- 2,562
- 3,715
Umechoka kunywa chai na vitafunwa vya aina moja kila siku leo pika vitumbua venye radha tofauti ufaidi chai yako ya asubuhi:
Mda dakika 50
Vipimo
Unga - 2 gilasi(wa mchele)
Mayai - 4
Hamira - 2 vijiko vya chai
Maziwa ya maji - 2 gilasi
Namna Ya Kutayarisha Na Kupika
- Weka mayai katika bakuli kisha yachanganye vizuri.
- Tia maziwa koroga.
- Tia hamira, koroga.
- Tia unga uchanganye vizuri.
- Weka uumuke, ukiwa tayari choma/pika kama unavyopika vitumbua vya kawaida.
- Vikishapoa weka kwenye sinia na mimina shira ukipenda vikiwa tayari kuliwa.