Mkuu tatizo la Bongo movie wanaigiza Mambo ambayo hayapo kwenye jamii yetu ndiyo maana Bongo movie imekufa, yani ukiangalia Movie zao wanavyoigiza tu kuanzia Nyumba na maisha ni tofauti na maisha yetu Wananchi Watanzania. Mfano Wanaigiza mambo ya jini na majumba mazuri na familia ya wazazi ukiangalia hao wazazi walivyo tofauti na jinsi wazazi wanayoishi Tanzania.Zimejiua zenyewe Mkuu
Hata Bongo Movies walikariri kila wakiigiza ni mapenzi tu sasa wapo wapi
Acha ujuajiWe jamaa huends hauna uelewa na hicho unachotaka kueleza au umechanganya mambo makusudi. Ubora hauna uhusiano wowote na Kizazi cha Gn Z kila generation inahitaji ubora. Usasa maana yake kuendana na watu wa sasa haina uhusino wowte na ubora labda uzungumzie kuhusu nature ya maudhui. Hivi vyombo vina wataalamu kuliko wewe na wanajua ni Traffic wanayoilenga
eti nitulie kuangalia jungu kuu hahahahaTatizo content packaging, we kituo cha TV kinarusha content hazina hata mvuto, ubora wa picha duni, ubora wa maudhui duni nk
Mkuu wanatakiwa wabadilike mbona Ulaya mpaka leo TV stations zipo na hazijafa, wao wanatakiwa wasogee mbele wasibaki walipo, wanatakiwa wawe wana Tangaza habari live kama wenzao wa Ulaya, Siyo Bus limepata ajari Same watu 45 wamekufa wao wanasubili saa mbili usiku kuonyesha.TV na redio sio biashara ya kufanya kwa sasa.
It's matter of time, TV na redio zinaenda kupotea.
Ndani ya miaka 10 kutoka leo, TV itabaki historia kama vitu vingine vingi vilivyopotea.
Habari ya mjini ni sosha network, wewe kama nimtangazaji wa TV ama redio, anza kujiwekeza kwenye akaunti zako za kijamii, tafuta followers kwa hali na mali.
Yaani kitu kinatokea sasa hivi na watu sasa hivi wanakishea, dunia nzima inapata habari, halafu wewe baadae saa mbili kamili usiku ndio unakuja eti kuanza kunisimulia kitu ambacho tayari nimeshakiona tangu mchna?
Nikae nipige simu redioni kuomba wimbo wa bestnasso wakati ninaweza nikauplay youtube, waste of time.
Mpaka BBC wana akaunti X, we huogopi?
Mfumo ndiyo unataka media ziwe hivyoYes Ila kwa Tanzania hali imebadilika.
Mfano radio watu wanasikiliza
vipindi Vya michezo
Na muziki .
Ni ngumu umkute kijana anafatilia Bunge , Taarifa ya habari.
Kwahiyo point sio kusikilizwa Sana je hao wasikilizaji wanasikiliza nn.
Wale watu unakuta from morning to evening anasililoza radio Fulani kwa sasa wamepungua .
Mtririko upo hivi
MTU anaamka na clouds michezo ikiisha anahamia , Wasaf ikiisha anahamia Crown ikiisha anahamia mjini Fm. N.k
Anzisha chako mwana. Utapiga hela si kitoto!Vipindi vyenu vipo kizamani sana!
Havina mvuto kwa kizazi cha sasa – yaani Gen Z.
Maudhui hayajawianishwa na ladha ya kidijitali/Kisasa, kasi ya dunia ya leo, wala ubunifu unaohitajika kuvutia vijana wa sasa.
📉 Tunashuhudia vipindi visivyoendana na mitindo ya sasa – havina mvuto wa picha, vina maigizo yaliyopitwa na wakati na havioneshi maisha halisi ya vijana wa leo. Kimbilio ni Pay TV Azam kule na MultiChoice angalau packaging yao ya content inavuta hadhira kwa namna fulani.
🔍 Jifanyieni tathmini ya kina – zungumzeni na watazamaji, tafuteni maoni yao, kajifunzeni kwingineko duniani muangalie data za utazamaji.
Gen Z wanahitaji maudhui ya kisasa, yanayoburudisha lakini pia yanaelimisha au mix ya both edutainment and infotainment yakiwa pachakaged kwa ubunifu wa hali ya juu na wa kisasa.
🎯 Fanyeni maboresho makubwa:
Kizazi cha leo hakiketi kuangalia kitu kisichokisisimua – kitafunga runinga na kuhamia TikTok, YouTube au Netflix.
- Ongezeni ubora wa picha (HD/4K). Acheni ubahiri walipeni Multiplexers wenu wawabebe kwenye quality nzuri nanyi badilisheni teknolojia na set za studio zenu. Mfano ITV hiyo studio ya Habari ni old school kitambo sana.
- Badilisheni watangazaji wekeni wenye mvuto, vituo karibia vyote havina watangazaji HB wala beautiful, wapo wababa na wamama, TV is all about attraction.
- Tengenezeni vipindi vya kisasa, vya kuvutia, vya haraka, vya kweli
- Toeni majukwaa ya ushiriki wa vijana – siyo vipindi vinavyowazungumzia na kuwabonda tu bali vinavyowahusisha na kuwaona wao pia ni sehemu ya jamii.
Pia rusheni maudhui yenu kwenye majukwaa yote muhimu kuwafikia vijana.
Muda ni sasa – jipangeni upya kabla hamjapoteza kizazi kizima cha watazamaji. CHANGAMKEENIII!!
MAONI HAYAPIGWI NYUNDO, HUFANYIWA KAZI!!!
HIVI TV1 Ilienda wapi walikuwa wabunifu sana wale jamaa!
N'yadikwa
Kwani Azam no DH? Na kama HD mbona Ukiangalia mechi kupitia Azam picha inakua tofauti na Ukiangalia Dstv, Dstv inaonyesha picha nzuri sana.Kila zama na nabii wake sasa ni zamu ya azamtv
usiwalaumu azam mfano uwanja wa lake tanganyika ni vigumu kupata picha nzuriKwani Azam no DH? Na kama HD mbona Ukiangalia mechi kupitia Azam picha inakua tofauti na Ukiangalia Dstv, Dstv inaonyesha picha nzuri sana.