Bookkeeping
Member
- Jun 6, 2025
- 75
- 169
hasa itv poor HD kabsa mtu anaonekan sura imejikunja kam amekatwa
Sijui kwa nin wanapata SUPER BRAND maana wamejichokeahasa itv poor HD kabsa mtu anaonekan sura imejikunja kam amekatwa
Hivi mnafuatilia vipindi vya tv?!Vipindi vyenu vipo kizamani sana!
Havina mvuto kwa kizazi cha sasa – yaani Gen Z.
Maudhui hayajawianishwa na ladha ya kidijitali/Kisasa, kasi ya dunia ya leo, wala ubunifu unaohitajika kuvutia vijana wa sasa.
📉 Tunashuhudia vipindi visivyoendana na mitindo ya sasa – havina mvuto wa picha, vina maigizo yaliyopitwa na wakati na havioneshi maisha halisi ya vijana wa leo. Kimbilio ni Pay TV Azam kule na MultiChoice angalau packaging yao ya content inavuta hadhira kwa namna fulani.
🔍 Jifanyieni tathmini ya kina – zungumzeni na watazamaji, tafuteni maoni yao, kajifunzeni kwingineko duniani muangalie data za utazamaji.
Gen Z wanahitaji maudhui ya kisasa, yanayoburudisha lakini pia yanaelimisha au mix ya both edutainment and infotainment yakiwa pachakaged kwa ubunifu wa hali ya juu na wa kisasa.
🎯 Fanyeni maboresho makubwa:
Kizazi cha leo hakiketi kuangalia kitu kisichokisisimua – kitafunga runinga na kuhamia TikTok, YouTube au Netflix.
- Ongezeni ubora wa picha (HD/4K). Acheni ubahiri walipeni Multiplexers wenu wawabebe kwenye quality nzuri nanyi badilisheni teknolojia na set za studio zenu. Mfano ITV hiyo studio ya Habari ni old school kitambo sana.
- Badilisheni watangazaji wekeni wenye mvuto, vituo karibia vyote havina watangazaji HB wala beautiful, wapo wababa na wamama, TV is all about attraction.
- Tengenezeni vipindi vya kisasa, vya kuvutia, vya haraka, vya kweli
- Toeni majukwaa ya ushiriki wa vijana – siyo vipindi vinavyowazungumzia na kuwabonda tu bali vinavyowahusisha na kuwaona wao pia ni sehemu ya jamii.
Pia rusheni maudhui yenu kwenye majukwaa yote muhimu kuwafikia vijana.
Muda ni sasa – jipangeni upya kabla hamjapoteza kizazi kizima cha watazamaji. CHANGAMKEENIII!!
MAONI HAYAPIGWI NYUNDO, HUFANYIWA KAZI!!!
HIVI TV1 Ilienda wapi walikuwa wabunifu sana wale jamaa!
N'yadikwa
Tena presenters ndiyo Kwisha kabisa.Quality iko chini sana. Wakati huo kilikuwa motoo. Ukunguukungu mwingi set za kizee, presenters wenye talent kwishaa, grafix za kizamani wakati huyu alikuwa mbabe wa grafix
Hivihivi vipindi vya kaa hapa nikae pale tuzungumze ambavyo ndiyo vimetawala TV stations zetu!? Nenda kule YouTube kaangalie TV programs zinaitwa Made in Tanzania au nenda hukohuko YouTube kwenye page ya The Citizen TV Kenya kaangalie mfano wa vipindi bora. Hapa Bongo hatuna vipindi vya TV vya kueleweka kidoogo anajitahidi UTV hawa wengine bado sana...Hivi mnafuatilia vipindi vya tv?!
Moja ya sababu hata vyanzo vya taarifa vinagoma kushiriki maana wanajua utatokezea kama kikaragosi quality ni mbovu sana. Nani anatazama video ktk SD quality zama hizi! Hiyo HD tu bado watu wanaona imepitwa na wakati watu wapo Ultra HD vituo vyetu vinaonesha SD, tunafeli sana!hasa itv poor HD kabsa mtu anaonekan sura imejikunja kam amekatwa