Vituo vya kujaza CNG kwenye magari vinavyotembea vitasaidia kujaza CNG kwenye magari kwenye mikoa mbalimbali

Nimeshakuelewa, ndo maana nimesema bado utahitaji vituo zaidi vya kujaza zaidi kile kimoja cha ubungo ambacho kitakuwa kinayajaza hayo malori yanayotembea, mchina mwenyewe huwa anaenda kujaza pale ubungo ndo anakuja kujaza Tazara.
Hapo nimekupata boss. Ila hiyo sio tatizo sana. Inaweza kutatuliwa. Changamoto ni kuipeleka hiyo CNG mikoani ndio inahitaji haya magari maalumu..
 
Kwani hamuwezi kujenga vituo vya CNG kama vya petrol station mnasupply iyo CNG kwa malori maalum sisi watumiaji tunaenda kwenye hivyo vituo tunajaza na kuondoka nadhan kutumia gari maalum litoe huduma itakuwa changamoto
 
Kujenga vituo inawezekana na ndio kinachofanyika saivi ila itachukua muda mpaka huo mradi uweze kukamilika
 
Kabla ya kuja na hii njia, ilipasa tujue soko la magari yanayotumia CNG limekua kwa asilimia ngapi?, Je nini kitatokea katika soko hilo kwa miaka 10-20 ijayo?

Dunia sasa inahama kitoka ICE kwenda kwenye Evs, lakini sisi kama Tz ndio kwanza tunawaza gas powerd vehicles, hauoni kama tuko nyuma ya muda?
 
Magari mengi yanabadirishwa Tanzania saivi boss. Ukienda kwenye vutuo vya kujaza gesi utakutana na msululu wa magari. Watu wana enjoy fuel economy.

CNG na EVs ndio main option ya kutunza dunia yetu zidi ya hewa ya ukaa. Karibu boss.
 
Nakukumbusha tena nyumba yako itakua salama endapo kama mtungi wa gesi ya kupikia (LPG) utahifadhiwa mahali penye hewa ya kutosha nje ya nyumba yako, na kupitisha mpira wa gesi kupitia ukutani au dirishani mpaka kwenye jiko lako jikoni.

Wahuni wataibaaa
 
Kwa nchi hii utelekelezaji unaweza ukaanza vizuri. Watu wakahamasika kuweka mitungi kwenye magari yao. Lakini kwa utendaji wa hawa viongozi. Mwisho utajikuta hiyo huduma unaingaikia mwenyewe,haipo tena. Mfano utajikuta unatoka mbeya kwenda dar,unaishiwa gesi katikati ya kitonga au iyovi au mikumi utajikuta unaisubiri gari la gesi siku 3. Au iwe biashara huria
 
Wabongo wana nyuzi zao bana!!?
hizi za maendeleo huwezi wakuta. Ww waambie mke wa Masanja kachepuka utakuta hao kibao!?
Ni kweli boss
 
Back
Top Bottom