Vituo vya mafuta katikati ya mji na makazi ya watu Dar: Bomu linalosubiri maafa makubwa

Nimeona sheria ya sasa inasema mita 200[emoji848] bado nina mashaka na hii sheria ni mita 200 toka makazi ya watu au kituo hadi kituo?
Kituo hadi kituo. Wasipojenga kwenye makazi watajenga wapi industrial area? Ukitaka kujaza mafuta uende industrial area. Kutoka Tegeta Hadi Posta barabara ile ina makazi 90% ya urefu wake je isiwe na kituo cha mafuta?
 
By the way uchawi na milipuko wapi na wapi?[emoji848][emoji848][emoji848]
Nilikuwa mfuatiliaji mzuri wa vipindi vilivyokuwa vinayotolewa na wataalam kutoka BP enzi zile ITV ndio nilijifunza hilo la umbali baada ya mdau mmoja kuuliza akitolea mfano wa vituo vya pale Fire kisha Magomeni na Mwembechai
 
Kituo hadi kituo. Wasipojenga kwenye makazi watajenga wapi industrial area? Ukitaka kujaza mafuta uende industrial area. Kutoka Tegeta Hadi Posta barabara ile ina makazi 90% ya urefu wake je isiwe na kituo cha mafuta?
Nimelinganisha na nchi nilizowahi kutembelea ... Vituo vya mafuta viko nje ya miji na naamini unajua ya kwamba tangu kuwaka taa ya tahadhari ya kuongeza mafuta basi una uwezo wa kwenda kilometer zisizopungua 30 mpaka gari lizime kabisa
 
Ardhi kununua haipungui milioni 500, au nao sio ktk mtaji
Hiyo 500mill kama unataka kuweka mjini ushindane na tajiri victoria mlokole mwenzangu anayeogopeka kwa mtaji mkubwa katika biashara ya mafuta.
Nenda nje ya mkoa viwanja vya milioni 5,kumi nk ila uwe na pesa ya kutosha maana kulipia bango tu lile la kusajiri mradi inaweza kukucost milioni 5 bado environment assessment etc ni kweli pesa ndefu?
 
Zamani nafikiri ilikuwa 1km kituo hadi kituo.
 
Nimelinganisha na nchi nilizowahi kutembelea ... Vituo vya mafuta viko nje ya miji na naamini unajua ya kwamba tangu kuwaka taa ya tahadhari ya kuongeza mafuta basi una uwezo wa kwenda kilometer zisizopungua 30 mpaka gari lizime kabisa
Sio lazima nimeona vingi tu nje ya nchi vipo karibu na makazi kabisa. Supermarkets nyingi zina vituo vya mafuta na zipo kwenye residential areas.
 
Hadi uanze kununua hayo mafuta unatakiwa ujenge hiyo petrol station yenyewe. Minimum lazima na Kama 400 million hapo unakuwa na machine Kama 4
Mashine pampu? Pampu moja milioni 15 ukitaka nzuri
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…