Vituo vya TV vimenibania kucheza video ya wimbo wangu "Usiunyanyape Moyo Wangu"

Vituo vya TV vimenibania kucheza video ya wimbo wangu "Usiunyanyape Moyo Wangu"

Civilian Coin

JF-Expert Member
Joined
Dec 2, 2012
Posts
2,305
Reaction score
4,380
Mimi Deogratius Nalimi Kisandu kwa jina la kisanii naitwa 'Masqo' mwaka 2005 niliingia Studio za SEI RECORD zilizopo Kinondoni chini ya Prodyuza SEIBLAT(Said) na kurekodi wimbo wangu unaoitwa "USIUNYANYAPAE MOYO WANGU" na nikafanikiwa kutengeneza Video yake na Prodyuza wa video Bw.MOSE pale Kariakoo, Dar es salaam.

Wimbo wangu ulibaniwa sana redioni lakini kwa msaada wa Kampuni ya JAPANTECH LTD iliyokuwa Vingunguti kwenye jengo la St.Joseph University walinisaidia kupata Promo kwa nguvu kubwa TBC FM chini ya Dijalo Alungu mpaka uzinduzi wa Albam yangu uliofanyikia TRAVENTINE HOTEL pamoja na Saida Karoli na H.Mbizo.

Pamoja na yote Televisheni ya C2C ya jiji Dar ilinisaidia kuupa Promo video yangu ya "Usiunyanyapae Moyo wangu" tangu 2005-2007 hivi, na Star Tv nao walianza kunipa Promo ya video hii kupitia Mtangazaji wa kituo hicho Bw. Nyanda. Nilijaribu kupeleka vituo vingine vya redio na TV lakini hazikupigwa nilibaniwa mpaka nitoe fedha, kimsingi mziki wa Tanzania umejaa unafiki na ukiritimba unaotakiwa kukomeshwa.
====================

Mwaka Juni 2014 nikiwa jijini Mwanza nilibadili gia aridhini na kuanza kuimba mziki wa Injili Mimi Deogratius Nalimi Kisandu nikitumia jina langu halisi badala yalile la kisanii "Masqo". Nilianza kwa wimbo wa "Yesu Umeniokoa" na baadae "Mama yangu Tanzania" na baadae "Sambaratisha Bwana Yesu" na "Katika Ndoa yenu" na "Yesu Atosha" na "Wewe ni Mungu" na "Dunia Mamba".

Baadae niliongezea wimbo mpya wa "Shangilieni" na baadae "Safari hii" na "Tumsifu Yesu Kristu".

Nilichoshangaa nyimbo zangu kupigwa nimpaka wakurugenzi wa redio niwapoze na rushwa kwanza ndio wawaambie Watangazaji wapige, nimejaribu kuwaomba waziingize kwenye system ili Redio zote wazipate laikini wamekuwa wagumu, nimeshuhudia vijana waimbaji wakienda kwa waganga kila kukicha ili wapate Promo na kung'aa, pia wamekuwa wakipandikizana chuki wao kwa wao na kuzimana huku wakiuana.

Kuna haja ya kutafakari nini maana ya Dini kama mimi naleta nyimbo zangu hamtaki kuzipiga mpaka niwe muumini wa Kanisa fulani ili hali sisi wote ni WAKRSTU?

DEOGRATIUS NALIMI KISANDU a.k.a Masqo
7 Desemba 2017.
 
Mziki biashara siku hizi lazima uwe na hela ya kutosha atiiii au tembelea nyota ya wakongwe kama anavyofanya billnas kajipendekeza kwa TID alipoona hana muelekeo akaenda kwa mwingine maarufu zaidi so cheza karata zako vizuri
 
MZIKI WA INJILI (GOSPO) UNAHITAJI NGUVU ZA GIZA ILIKUPIGWA REDIONI.

Mwaka Juni 2014 nikiwa jijini Mwanza nilibadili gia aridhini na kuanza kuimba mziki wa Injili Mimi Deogratius Nalimi Kisandu nikitumia jina langu halisi badala yalile la kisanii "Masqo". Nilianza kwa wimbo wa "Yesu Umeniokoa" na baadae "Mama yangu Tanzania" na baadae "Sambaratisha Bwana Yesu" na "Katika Ndoa yenu" na "Yesu Atosha" na "Wewe ni Mungu" na "Dunia Mamba".

Baadae niliongezea wimbo mpya wa "Shangilieni" na baadae "Safari hii" na "Tumsifu Yesu Kristu".

Nilichoshangaa nyimbo zangu kupigwa nimpaka wakurugenzi wa redio niwapoze na rushwa kwanza ndio wawaambie Watangazaji wapige, nimejaribu kuwaomba waziingize kwenye system ili Redio zote wazipate laikini wamekuwa wagumu, nimeshuhudia vijana waimbaji wakienda kwa waganga kila kukicha ili wapate Promo na kung'aa, pia wamekuwa wakipandikizana chuki wao kwa wao na kuzimana huku wakiuana.

Kuna haja ya kutafakari nini maana ya Dini kama mimi naleta nyimbo zangu hamtaki kuzipiga mpaka niwe muumini wa Kanisa fulani ili hali sisi wote ni WAKRSTU?

DEOGRATIUS NALIMI KISANDU a.k.a MASQO
7 Desemba 2017.
 
Back
Top Bottom