Vituo vya Yatima (Orphanages) ni biashara ya utumwa

Hii ni sahihi kabisa, Mamlaka zifanye intervention ikiwezekana ipatikana Sheria ya kuguide izi Centers aisee mana the situation is very worse now, Nina ushahidi na opharnage centers mbili that business pays
Ila bibi Kizee Faiza, Mtoto ni mtoto hakuna mtoto Haramu
Kids are innocent regardless wamepatikana kwa Njia ipi
 
Hakuanaga watoto haramu regardless wamezaliwa katika mazingira yapi, binadamu ni binadamu tuu.

Acha kukufuru wewe bibi, hata wewe huwezi jua huenda mama yako alibakwa au alichepuka nje ya ndoa ndiyo ukazaliwa wewe.
Waislam ndiyo wanapenda kutumia maneno hayo mtoto wa nje ya ndoa mtoto haramu, mtoto ambaye bibi zake wa upande wa baba hawampendi na hawana furaha nae.
 
Vingi vimejaa watoto waliopatikana kwa njia haramu (watoto wa zinaa na uasherati).

Mpuuzi sana wewe, imani yako isikufanye ukose utu kwa mtoto asie na kosa. Toa hukumu yako kwa mzazi na si mtoto asie na hatia
Kwa sheria za uislamu imefafanua mtoto wa nje ya ndoa na mtoto wa ndoa, Uislamu umemnyima haki zote kutoka kwa Baba mzazi na imempa haki kutoka kwa Mama yake mzazi, mfano mirathi, Majina, Mtoto wa nje ya ndoa kwa waislamu mtoto anakuwa wa mama pekee ndiyo maana anatumia Majina ya Mama na hatumii majina ya Baba yake mzazi, na kwenye urithi wa mali za baba yake yeye hatakiwi kuithi mali za marehemu baba yake, na mfano Baba yake amefariki ikifika muda wakutaja wasifu wa marehemu kwenye kipengele cha kutaja idada ya watoto wa marehumu mtoto wa nje ya ndoa hawatajwi, we utasikia marehemu kaacha wake watatu na watoto 10, saa watoto kumi ni wale walio zaliwa ndani ya ndoa tu ndiyo wanatajwa.
 
Mwanzo 21:9-11

"Sara akamwona yule mwana wa Hajiri Mmisri, ambaye alimzalia Ibrahimu, anafanya dhihaka. Kwa hiyo akamwambia Ibrahimu, Mfukuze mjakazi huyu na mwanawe, maana mwana wa mjakazi hatarithi pamoja na mwanangu, Isaka. Na neno hilo lilikuwa baya sana machoni pa Ibrahimu, kwa ajili ya mwanawe"

.
 
huwa najisikia AIBU sana kukuta mtu kama wewe anaongea vitu ambavyo hana facts navyo
 
A child is born with no state of mind Blind to the ways of Mankind.
 
Kuna kituo cha mayatima huku zanzibar kilitembelewa na Makamu wa pili wa Rais wa Zanzibar. Kuna mtt maneno aliyoongea nililia km mtoto juu ya wanayofanyia na mama walezi wao.

Dada Faiza umeongea ukweli mtupu. Inataka imani thabit kukaa na wtt yatima na kuwa muadilifu kwenye misaada wanayopatiwa
 
Kwa uzoefu wangu hasa vituo vya Da es salaam kile kilichopo Kigogo -Mburahati, Kilichopo mitaa ya Karume karibu na Kigogo Sambusa, pale Kibada eneo la Mwafrika, na vingine vingi ni miradi ya kuendeleza umaskini: Hawa watu wana ndugu , jamaa na marafiki, hawataki ila wanataka kutupa watoto humo vituoni, hili jambo tukisubiri serikali itachukua miaka mia , we should wake up as a community.
 
Vyote ni biashara ya utumwa.

Hivi vituo vina mambo mabaya sana yanaendelea. Mengine hayasemeki.

Watu wa ustawi wa jamii wanaelewa kabisa, lakini nao ni miradi yao, kazi yao kwenda kuchukuwa posho kila kituo na kutoka kwa wafadhili, huwa wanachukuliwa kama tour guide ili wafadhili wenye nia ovu wapate kinga ya kuwa wameenda kiserekali.

Vikundi vya kueneza ushoga na usagaji siku hizi ndiyo sehemu zao, hawaishi huko.


Jamii inabidi kweli tufanye kazi, tusiingoje serikali.
 
Tatizo huyu bibi huandika kwa mihemko., kuna watu huwa wanajiona kabisa wako perfect na Mbingu ni yao while not.
 
Ni tusi kwa utu damu na uhai kwa ujumla.Ni kosa kutukana kiumbe kilichozaliwa kihalali kabisa.
 
Kwanini basi kujadili mada ya mtu mbabe na mkorofi namna hii.Ila tuendelee pengine ni yatima.
 
Hapa dada tunashare interest kubwa mm ni mdau wa kulea yatima .
Uliyosema nathibitisha 100% nimeyaona ni miradi ya watu kabisa .ila nimekuja na namna yangu nawafikia hasa watoto wanaoishi mazingira magumu.
 
Ni tusi kwa utu damu na uhai kwa ujumla.Ni kosa kutukana kiumbe kilichozaliwa kihalali kabisa.
Hakuna aliyetukanwa. Mtoto aliyepatikana kwa njia za haramu anaitwa "mwana haramu", hilo halimaanishi kuwa huyo mtoto ndiyo haramu, linamaanisha kapatikana kwa njia za haramu.
Hapa dada tunashare interest kubwa mm ni mdau wa kulea yatima .
Uliyosema nathibitisha 100% nimeyaona ni miradi ya watu kabisa .ila nimekuja na namna yangu nawafikia hasa watoto wanaoishi mazingira magumu.
Mwenyezi Mungu awafanyie wepesi.

Kuna watoto humo mpaka wa baba zao.
 
Zinaa na uasherati ni haramu, lakini mtoto, bila kujali jinsi alivyopatikana si haramu.

Kuna watoto yatima wanaoishi ambao japo hawaishi kwenye vituo vya watoto lakini wana maisha mazuri kuliko baadhi ya watoto wanaoishi na wazazi wao.

Vituo vya watoto yatima ni jina lililozieleka, lakini jina sahihi zaidi ni VITUO VYA KULELEA WATOTO WANAOISHI KATIKA MAZINGIRA MAGUMU.

Kwa hiyo basi, vituo hivyo huweza kuwapokea watoto wote waliothibitishwa kuwa na uhitaji huo:
1. Yatima waliokosea ndugu wa kuwalea

2. Watoto wanaoishi mitaani kutokana na matatizo ya kifamilia kama wazazi kuachana n.k.
Na kabla ya watoto kupokekewa vituoni, huthibitishwa kwanza na ustawi wa Jamii.

Mkuu, uwe unapeleka alu bokdi Moja la sabuni kwenye hivyo vituo, vingi vina uhitaji kuliko inavyofikiriwa.
 
Yaani mchakato wa kumpata mtoto umetengenezwa na Mungu ..afu mtoto aliyepatikana Kwa mchakato uleule anaitwa haramu?! Rubbish ...yaani tunampangua Mungu
 

Mtoto wa uzinzi na ushaerati kapatikana kwa njia za haramu. Mtoto mwenyewe siyo haramu, waliompata ndiyo walifanya haramu.


Hao watoto wapo mpaka wa kaka zao, baba zao, wajomba zao, babu zao.

Kama hawajapatikana ki haramu ni nini hicho kitendo?
 
Yaani mchakato wa kumpata mtoto umetengenezwa na Mungu ..afu mtoto aliyepatikana Kwa mchakato uleule anaitwa haramu?! Rubbish ...yaani tunampangua Mungu
Labda huna dini. Uislam umekataza kuzaa nje ya uliohalalishiwa kuwaoa, kinyume cha hapo unafanya haramu.
 
Hakunaga mtoto anayezaliwa kwa Njia haramu wala hakuna mtoto haramu hata kidogo. Hiyo statement yako ndio haramu.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…