inspectorbenja
JF-Expert Member
- Oct 14, 2012
- 597
- 651
Gari iko Ifakara Mjini ya wapi Afande? Viwanja 60, Silent Inn, Mlabani, Mwembetogwa, Kwa Shungu, Lipangalala, Katindiuka, Lumemo!Habari wadau.
Nina gari Vitz old model. Engine yake inasumbuasumbua inahitaji either fundi makini au half engine au engine mpya.
Half engine nimeambiwa mil 1. Engine kamili mil 2. Mimi nimefulia hata ipite miaka kadhaa sitakiwa na uwezo wa kuinunua. Hivyo naiuza.
Mimi ndo mmiliki siyo dalali. Bei maelewano ila-gari ipo Ifakara mjini
Kaka unasema kweli.Mafundi wanaigusa sana lakini bado inasumbua.Gari iko Ifakara Mjini ya wapi Afande? Viwanja 60, Silent Inn, Mwembetogwa, Kwa Shungu, Lipangalala, Katindiuka, Lumemo!
Halafu VITS ikishazingua injini, dawa yake ni kubadilisha tu. Kinyume na hapo utaliwa hela weee mpaka ujute kuifahamu.
Hivi vigari ni vigumu sana. Ila changamoto yake kubwa ni hiyo kwa baadhi ya injini zake. Yaani ikizingua, ni kununua tu injini used. Ukifunga, ni mkataba.Kaka unasema kweli.Mafundi wanaigusa sana lakini bado inasumbua.
Gari ipo Kibaoni.
Enhe tunapozana bei Gan hapa??