Wewe jamaa sababu zako hata hazieleweki. Na haziingii alilini mwa mtu anayeangalia na mpemzi wa soka. Guardiola CV yake kwa barcelona ni undisputed,
Kuachwa kwa mchezaji katika kikosi inategemea na kocha anahitaji timu icheze mpira wa aina gani. Na si mara zote kwamba yule anayeanza ni bora kuliko yule aliye nje. Mfano, kuna baadhi ya mechi za Elclassico Ramos, Pepe walipata kucheza namba 6 chini ya mourinho na Anceloti.
Mascherano kwa sasa anacheza namba 4 muda mwingi na mechi nyingi, ila ni mara nyingi sana Mascherano huwa anafuta makosa ya Busquets kwa kufanya interceptions zilizotukukuka ambazo ni dhahiri huwa zinaonekana zinatokea kwa kufail kwa namba 6.
Usichokijua ni kwamba, Busquets anafichwa na mfumo wa timu wa kumiliki mpira hivyo kufanya most of the time awe na mpira na arelax akiwa na mpira, ila ikitokea timu inashambuliwa muda mwingi, mascherano ni undisputed katika kuzuia mashambulizi.
All in all inategemea namba 6 huyo kakabidhiwa majukumu gani, Usikariri mpira. Mpira unaenda kwa facts na majukumu, kila mtu ana majukumu yake ya msingi awapo uwanjani na namba 6 jukumu lake la msingi ni kulinda central backs zisifikiwe na adui kiurahisi, na jukumu hili la namba 6 most of the time linapimwa pale timu inapokuwa inashambuliwa na si kushambulia, busquests kwa hili anafeli pakubwa.