Viungo gani vinafanya nyama kuwa laini na yenye ladha?

Na yale makamba kamba ya tangawizi unayachemshia huko au unaikamua ili upate maji tu
Ninapenda tangawizi, mradi tu siweki nyingiiii hadi kukera. So, nikiwa na muda ninachuja, kama sina naponda kwa kijikinu changu kidogodogo ama nakwangua kwa grater natupia kwa chungu changu
 
Na yale makamba kamba ya tangawizi unayachemshia huko au unaikamua ili upate maji tu
Kama huyapendi hayo, andaa tangawizi yako uikatekate au iponde kwenye kinu kiasi then blend.
 
Jamani
Soy sauce imenishinda
Sijui Ndo ushamba
Saga kitunguu na nyanya kwa pamoja then kaangaa vikiiva weka soya sauce changanya then paka kuku, nyama, samaki ikiwa mwishoni kuiva wakati wa kuchoma au weka soya sauce kwenye makange bila mchuzi.
 
Nawasilimu kwa jina la jamhuri ya Muungano wa Tanzania.

Naomba kujuzwa unapotaka kupika nyama yako (mfano; ya ng'ombe au Kuku) ni viungo vipi ukichanganya wakati wa kuchemsha nyama hiyo itaifanya kuwa yenye ladha na laini?

Asante.
Tumia slow cooker weka kitunguu swaumu na tangawizi weka kwenye slow cooker nyama inakolea viungo na kuwa tamu na kama huna slow cooker unaweza kutumia chupa ya chai zile za chuma weka huko nyama kama masaa sita au usiku kucha nyama inakolea viungo inakuwa tamu hata usipounga.
 
Saga kitunguu na nyanya kwa pamoja then kaangaa vikiiva weka soya sauce changanya then paka kuku, nyama, samaki ikiwa mwishoni kuiva wakati wa kuchoma au weka soya sauce kwenye makange bila mchuzi.
unatumia brand gani?
au zote ni sawa tu?
 
Tumia slow cooker weka kitunguu swaumu na tangawizi weka kwenye slow cooker nyama inakolea viungo na kuwa tamu na kama huna slow cooker unaweza kutumia chupa ya chai zile za chuma weka huko nyama kama masaa sita au usiku kucha nyama inakolea viungo inakuwa tamu hata usipounga.
ooh this one
 
Viungo vya kitoweo cha nyama ni tofauti na kitoweo cha samaki.

Samaki ni laini usipokuwa makini analegea nakumomonyoka.
 
Back
Top Bottom