Viungo vitatu vinavyoharibu maisha ya wanaume wengi

Viungo vitatu vinavyoharibu maisha ya wanaume wengi

Gol D Roger

JF-Expert Member
Joined
Sep 16, 2023
Posts
2,316
Reaction score
6,082
Karibu...

1. MDOMO
Jifunze ku-control mdomo wako, mdomo unaharibu mdomo unatengeneza, unatakiwa ujue kutofautisha kati ya muda sahihi wa kuongea na muda wa kunyamaza na kusikiliza wengine. Usijiongelee mambo mabaya hata kama mnataniana na washkaji, jifunze kuwatamkia watu mema na kuwaambia ukweli.
Jitahidi kuweka vocabulary zako sawa kabla ya kuongea, usiwe mtu wa kutafuta maneno wakati unaongea, hii ni silaha kubwa sana na itakutofautisha na watu mengine.
Kumbuka pale tuu unapoamua kufungua mdomo wako na kuongea automatically unawaambia watu wewe ni mtu wa aina gani, so either utajiongezea heshima au utajipunguzia heshima.

2. TUMBO
Usiendekeze tumbo, sio kila unaposikia njaa unaharakisha kutafuta chakula, amini nakwambia unaulegeza mwili wako, jitahidi kufunga mara kwa mara, kufunga kunaimarisha sana mwili na kuuweka sawa.

Jifunze kutokuwa mtumwa wa tumbo lako na katika mambo ambayo inabidi uwe makini nayo ni aina ya chakula unachokiingiza tumboni, chakula ndo afya yako, so mind what you eat, aina na kiwango cha chakula unachokula kina impact kubwa sana kweny mabadiliko ya nishati ya mwili wako throughout the day, so avoid kula mavyakula yenye carbohydrates nyingi asubuhi, inasababisha insulin spikes ambazo badae inakuja ku-lower blood sugar then badae ikifika saa 6 tuu umechoka unaanza kupiga miayo.

Ukiweza ku-contol tumbo lako utajikuta siku nzima mwili una nishati ya kutosha na utaweza kufanya shughuli zako bila kuchoka.

3. UUME
Jifunze ku-control hisia za mapenzi ndugu yangu, yaan ukiweza ku-control hisia za kimapenzi hakuna kitu kitakushinda hapa duniani, hiki ndo kipengele kikubwa kwa wanaume wengi.

Wanaume tunapoteza muda na hela nyingi kwa kuendekeza kufanya mapenzi, tumekuwa watumwa hadi inafika hatua mtu anaamua kuchukua sheria mkononi, huo ni udhaifu ambao inabidi upambane nao, hata mbwa afanyi hivo, inamaana una akili ndogo kuliko mbwa??

Usikubali kuwa mtumwa wa viungo vyako mwenyew, Jifunze kuunyamazisha mdomo wako, usiendekeze tumbo, usikubali kuendeshwa na nyege, usiongozwe na mwili wako, ongoza mwili wako.
 
Back
Top Bottom