BigTall
JF-Expert Member
- Mar 9, 2022
- 525
- 1,257
Leo tarehe 19, Septemba 2024 mmoja kati ya Watoto wale mwili wake umeonekana maeneo fulani, Mwandishi wa MillardAyo.com akafika hadi eneo la tukio kwa ajili ya kurekodi tukio lote.
Wakati anaelekea kukamilisha kazi yake hiyo, kuna Watu wakajitokeza na kumvuta pembeni, tukaona purukushani kama vile wanabishana, baadaye yule ripota akatuambia wale watu wanadai wametumwa kutoka Ofisi ya Mkuu wa Mkoa wa Arusha.
Kumbe lile sekeseke la kimya kimya walitaka kumnyang’anya kamera, na kwa kuwa awali Watu hawakuwa wengi mwanzoni, ikatokea hali ya vuta nikuvute kwa dakika kadhaa.
Mwisho wake wale watu wamefanikiwa kuondoka na kadi ya kamera husika ambayo imerekodi tukio lote na sasa Wananchi tumebaki tunajiuliza kulikuwa na sababu gani ya hao watu kutaka tukio hilo lisirekodiwe.
==============
Mwandishi Wa habari Godfrey Ng'omba Ripoter Wa Millard Ayo - Arusha, leo Septemba 2024 amevamiwa na Askari Polisi Kwa maelekezo ya Mkuu wa Mkoa wa Arusha, Paul Makonda akiwa anarekodi tukio la watu kufunga Barabara ya Moduli kutokana na tukio la watoto wawili kupotea,polisi hao waliotaka kumpora camera alipo wazidi nguvu msaidizi mmoja Wa Makonda akashuka kwenye gari na kwenda kuwasaidia polisi akachoa Kadi ilivyokuwa kwenye camera yake na kuondoka nayo
wananchi hao walifungwa Barabara kumzuia Makonda asipite akiwa anaetokea kwenye ziara yake Monduli Hadi wapate majibu ya kupotea Kwa watoto hao tukio Hilo limetokea maeneo ya Mbuyuni katika Kata ya Makuyuni wilayani Monduli
Inaelezwa kuwa Makonda baada ya kufika na Msafara wake alipomuona mwandishi huyo Wa habari akiwa na camera yake aliwaagiza Askari wamkamte na kuzuia habari hizo za watu kufunga Barabara zisionekane kwenye Chombo chochote Cha Habari.