Narudia tena, usiwe mjinga tafadhali, achana na hizo nchi zinazofundisha kiswahili kama somo, hapa Tanzania elimu ya sekondari yote mpaka vyuoni masomo yote ni kwa kiingereza kasoro kiswahili chenyewe, lakini mtu anamaliza chuo kikuu hawezi kuongea kingereza (fluently English) cha kunyooka zaidi ya nusu saa. Mfano mrahisi ni huyo mzalendo wa kiswahili ana PhD, kiingereza chake sipendi kiwe mjadala hapa kwa heshima yake. Je itakuwa hizo nchi ambazo mtu anasoma somo la kiswahili tu, tena sehemu nyingine wanasema ni optional, ndio kuwe na waongea kiswahili?
Hizo nchi za SADC unazoambiwa blahblah ya kiswahili, watakaokuwa wanakiongea ni Magu na viongozi wachache watakaoandaliwa repoti waisome kwa kiswahili, na siku Magufuli akitoka madarakani hutaona mtanzania mwingine tena akiongea kiswahili kwenye hiyo mikutano ya SADC. Nchi za East Africa ambako Tanzania ndio kubwa, hata vikao vya hiyo jumuiya kiingereza ndio lugha kuu, na hata ukiongea kiswahili bado wengi wanapenda kiingereza kuwa ndio kinaeleweka zaidi. Waongea kiingereza humo kwenye hiyo jumuiya ni watanzania tena wale ambao kiingereza kinawasumbua, na Wakenya wachache tena nao ni kwakifupi sana. Narudia tena, dunia hiii waongea kiswahili hawavuki 70m, tena 88%+ ni watanzania, 10%+ ni wakenya, na hiyo % nyingine ni waliobakia.