Viwanda Gani Tanzania Vinatengeneza vifaa vya kujikinga (PPEs) kama barakoa, glovu n.k?

Viwanda Gani Tanzania Vinatengeneza vifaa vya kujikinga (PPEs) kama barakoa, glovu n.k?

Mojawapo ha changamoto kubwa zilizolefwa na baa la virusi vya korona Ni ukosefu au upungufu wa vifaa vya kujikinga binafsi. Glovu, kofia, barakoa, gauni Kinga no Ni baadhi tu ya vifaa hivi.

Mahitaji ya vifaa hivi duniani yameongezeka Sana. Katika Hali ya kufa kufaana me viwanda Gani Tanzania Vinatengeneza PPEs hizi na vinachukua hatua gani kutumia nafasi hii kufanya ugavi ndani na nje?
Mkuu kwema? Bora umetoa post maana nilianza kupata hofu! Leo kitu kinaenda 22K ila nakumbuka wiki mbili tu zilizopita walikuwa 8K na wiki tatu zilizopita walikuwa chini ya elfu moja. Corona haina tajiri wala masikini.

Bad
 
Mojawapo ha changamoto kubwa zilizoletwa na baa la virusi vya korona ni ukosefu au upungufu wa vifaa vya kujikinga binafsi. Glovu, kofia, barakoa, gauni kinga no ni baadhi tu ya vifaa hivi.

Mahitaji ya vifaa hivi duniani yameongezeka sana. Katika hali ya kufa kufaana me viwanda gani Tanzania vinatengeneza PPEs hizi na vinachukua hatua gani kutumia nafasi hii kufanya ugavi ndani na nje?
Mwanakijiji huko uliko, najua unachukua tahadhari zote lakini nakusihi chukua tahadhari mara 2 zaidi ya wazungu. Maana kwa taarifa rasmi inaonesha huko US by proportion, waliopoteza maisha, wengi zaidi ni ngozi nyeusi.
 
Vifaa vya kujikinga binafsi = Vifaa vya kinga mwilini
PPEs = PPE (Personal Protective Equipment)
Siyo PPEs!


Sent using Jamii Forums mobile app

Uko sahihi, neno equipment halina s mwishoni

Bado kwenye articles nyingi, websites na reports inaandikwa PPEs, s inakuwa ndogo na inabeba PPE yote

Ni un official emphasize ya wingi wa ppe ila acceptable sana tu
 
Mi nashangaa viwanda vinapandisha bei za bidhaa mf sukari sijui inahusiana vipi na korona!
Kuna mambo mengi yanachangia. Yawezekana hata namna wafanyakazi wanavyoenda kazini na kurudi majumbani kukawa na mipango maalum ambayo, mwisho wa yote huongeza gharama za uzalishaji.

Lakini pia wapo ambao hutumia kanuni zile za uchuni na biashara za demand and supply. Sahizi kuingiza sukari toka nje siyo rahisi kama zamani.

Tutarajie bei za bidhaa nyingi kupanda kwa sababu uzalishaji wa ndani ni duni sana.

Kila mara tumekuwa na mihemuko bila ya kuwa na sera ya viwanda inayoweza kusaidia kujengwa na kustawi kwa viwanda. Kodi, ukiwa na kiwanda ni zaidi ya 30 halafu utegemee kujengwa kwa viwanda!! Wawekezaji wengi hawawezi kujenga viwanda Tanzania eti kwa sababu Rais au waziri amesema. Wao huongozwa na Selection Criteria zao ambazo hupima mambo mengi kwa pamoja.
 
Mojawapo ha changamoto kubwa zilizoletwa na baa la virusi vya korona ni ukosefu au upungufu wa vifaa vya kujikinga binafsi. Glovu, kofia, barakoa, gauni kinga no ni baadhi tu ya vifaa hivi.

Mahitaji ya vifaa hivi duniani yameongezeka sana. Katika hali ya kufa kufaana me viwanda gani Tanzania vinatengeneza PPEs hizi na vinachukua hatua gani kutumia nafasi hii kufanya ugavi ndani na nje?
Hio ni fursa iliyo nje nje
 
Property ,Plant & Equipment - IAS 16 in accounting ( fixed assets) Or Personal Protective Equipment in health issue
Mnanichanganyia dawa sasa... Nilikuwa najua ya accounting standards nilipouliza nkapewa ya afya... In a we za kuwa kuna ya wale Wa kula kimasihara pia
 
Sisi hatuna uwezo au resources za kuzalisha hayo Material ?
Fanya tafiti mkuu me ninacho juwa material yana toka china!!!! Na machine na spear part za machine ingawaje na nchini nyingine pia ni ghali zaidi ya china!!
Mimi ni rafiki wa machine!
images (11).jpeg
 
Laiti wengetumia local materials kuliko kufanya assembling tu ya mask kama kile kiwanda cha wahindi.
Ni ngumu na gharama sana kupata mask tokea nje,Kwani kila nchi ina upungufu.
Nilitegemea viwanda vile vya Magufuli maarufu kama viwanda vya cherehani nne,vitengeze home made mask kwa matumizi ya dharura na kwa watu wengi.
 
Mojawapo ya changamoto kubwa zilizoletwa na baa la virusi vya Corona ni ukosefu au upungufu wa vifaa vya kujikinga binafsi. Glovu, kofia, barakoa, gauni kinga ni baadhi tu ya vifaa hivi.

Mahitaji ya vifaa hivi duniani yameongezeka sana. Katika hali ya kufa kufaana ni viwanda gani Tanzania vinatengeneza PPEs hizi na vinachukua hatua gani kutumia nafasi hii kufanya ugavi ndani na nje?
Hizi ndizo nyuzi tulizotakiwa kujadili mapema tu, badala yake ulianza na uzi wa kumsifia Magufuli kwa mikakati yake ya kupambana na COVID-19. Tulikupinga kwa hoja, na kwa kweli sasa inaonekana serikali ndio inaanza kuzinduka. Na nyie waimba mapambio mnashituka kumekucha.
 
Mojawapo ya changamoto kubwa zilizoletwa na baa la virusi vya Corona ni ukosefu au upungufu wa vifaa vya kujikinga binafsi. Glovu, kofia, barakoa, gauni kinga ni baadhi tu ya vifaa hivi.

Mahitaji ya vifaa hivi duniani yameongezeka sana. Katika hali ya kufa kufaana ni viwanda gani Tanzania vinatengeneza PPEs hizi na vinachukua hatua gani kutumia nafasi hii kufanya ugavi ndani na nje?
Hoja murua kabisa Mkuu, kipindi kama hiki miongoni mwa kazi za majeshi yetu kupitia vitengo vyake vya uzalishaji ikiwemo Magereza, Suma-JKT n.k zingalikuwa ni kujihusisha na uzalishaji wa vitu kama hivi.

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Mzee umegusia jambo kubwa.
Natamani vifaa hivi vingetengenezwa hapa nyumbani katika ubora tunaoutaka.
Ni jambo la msingi kwa security pia maana tayari vifaa vinavyotoka China vimeleta msuguano na mataifa ya Ulaya sababu vingi havina ubora.Kwa mfano Uingereza wamegundua vifaa zaidi ya mil 2.5 vinavyotumika kupimia havina ubora.Pia kwingineko wamegundua mask nyingi zinazotokea China zina nafasi kubwa ya kupitisha hewa isivyotakiwa na hivyo havitofaa kuzuia maambukizi ya hewa.Na nchi nyingi zinaanza kukataa vitu vya China.
Kama tunao uwezo kutengeneza haya ni heri tutengeneze.
 
Back
Top Bottom