Viwanda Gani Tanzania Vinatengeneza vifaa vya kujikinga (PPEs) kama barakoa, glovu n.k?

Viwanda Gani Tanzania Vinatengeneza vifaa vya kujikinga (PPEs) kama barakoa, glovu n.k?

Mwanakijiji huko uliko, najua unachukua tahadhari zote lakini nakusihi chukua tahadhari mara 2 zaidi ya wazungu. Maana kwa taarifa rasmi inaonesha huko US by proportion, waliopoteza maisha, wengi zaidi ni ngozi nyeusi.
Ni kwaaababu wengi wanaishi kwenye close quarters. Ndo maana hapo Dar nasikitika sana kina Makonda walileta siasa.
 
Mojawapo ya changamoto kubwa zilizoletwa na baa la virusi vya Corona ni ukosefu au upungufu wa vifaa vya kujikinga binafsi. Glovu, kofia, barakoa, gauni kinga ni baadhi tu ya vifaa hivi.

Mahitaji ya vifaa hivi duniani yameongezeka sana. Katika hali ya kufa kufaana ni viwanda gani Tanzania vinatengeneza PPEs hizi na vinachukua hatua gani kutumia nafasi hii kufanya ugavi ndani na nje?
Ndugu
Ningefurahi sana ungejikita na post yako kuhusu kamari ya Magufuli juu ya namna anavyoshughulika na janga la corona. .
Je italipa?
 
Laiti wengetumia local materials kuliko kufanya assembling tu ya mask kama kile kiwanda cha wahindi.
Ni ngumu na gharama sana kupata mask tokea nje,Kwani kila nchi ina upungufu.
Nilitegemea viwanda vile vya Magufuli maarufu kama viwanda vya cherehani nne,vitengeze home made mask kwa matumizi ya dharura na kwa watu wengi.
Nchi nyingi zina zalisha home made masks kwa gharama nafuu. Huku kwetu hatujui hata uwezo wetu wa kuzalisha upoje. Shida sana!
 
Ni wakati wa wewe na Dr Slaa kuueleza umma wa Watanzania kuhusu uongo wa Tanzania ya Viwanda , nafasi mnayo maana mko karibu na Utukufu wa Dunia .

Nchi ambayo haiwezi kutengeneza hata pamba za kuoshea vidonda ( bali inaagiza kutoka Kenya ) itaweza Barakoa ? na nakuhakikishia kwamba siku Tanzania ikitengeneza barakoa , ndio siku mtu akivaa atakufa hapo hapo kwa kukosa hewa .
 
Mojawapo ya changamoto kubwa zilizoletwa na baa la virusi vya Corona ni ukosefu au upungufu wa vifaa vya kujikinga binafsi. Glovu, kofia, barakoa, gauni kinga ni baadhi tu ya vifaa hivi.

Mahitaji ya vifaa hivi duniani yameongezeka sana. Katika hali ya kufa kufaana ni viwanda gani Tanzania vinatengeneza PPEs hizi na vinachukua hatua gani kutumia nafasi hii kufanya ugavi ndani na nje?

..wewe si ulikuwa unamsifia Jpm kuwa anacheza "BAHATI NASIBU" na covid19?

..nini kimekufanya ubadilishe mtizamo wako?
 
Back
Top Bottom