Ni kweli Viwanda alivyojenga Nyerere ni Vichache sana. Vingi vilijengwa na Wahindi na Wazungu. Alichofanywa Nyerere Chini ya Siasa ya Ukamaa na Kujitegemea ni kuviTAIFISHA(NATIONALISATiON). Yaani kuweka Chini ya Wazawa UMMA wa Watanzania. Tukashindwa kuendeleza Vikafa. Mfano wa Tanganyika Packers ya Kawe(Cow Way). Kiwanda kilisindika nyama ya kopo ikawa inauzwa Arabuni, Ulaya na USA. Mzungu wa kiwanda hiki alinunua Ngombe Usukumani, Tabora na Arusha. Alikuwa na Eneo maalum la kuwalisha kabla ya kuchinjwa. Nyumba za wafanyakazi na mengineyo. Kiwanda kilishamiri Biashara Safi. Hata Mimi nilikula nyama ya Kopo ya Kawe. WalivyoTaifisha tu Hadi Leo hakijawahi kufanya Kazi. Matokeo yake Eneo la Tanganyika Packers limekuwa Eneo la Mikuano ya Injili, Nyumba NHC zinajengwa pale, wauza Maua wanamiliki, stand ya Mabasi na shughuli nyingine. Kiwanda chetu cha Nyama tulikiua Sisi wenyewe Kisiasa. Tena wakati wakaanza kuzichakata. Wanasema ziliozea ndani pakanuka miezi 3. Mashine zake Sijui zilipelekwa wapi.
Balehe ya siku hizi nzuri sana ndio maana tunaakili na tunajua history vizuri,1970 Tanzania ilikua masikini wa kutupwa tulikua tumeua viwanda vyote!!!...mtu anayesema Nyerere alijenga viwanda nadhani hajui history vizuri (Nchi hii ni ya wakulima) wakati wa kupiga kura ya uhuru ilikua jumatatu siku ambayo watumishi wote wa serikali na viwandani walikua kazini!!
Soma history vizuri utajua hakuna kiwanda kilichojengwa na Nyerere vyote vili taifishwa!!!.. Cabinet ya Nyerere ndio ilikuja kuua vyote
Mfumo wa uchumi wa kimashariki (Kijamaa) kupitia Azimio la Arusha uliopora viwanda na Mali nyingi za matajiri na serikali kujimilikisha na kuviendesha.
Bahati mbaya viliendeshwa kwa kupangiwa bei na serikali bila kujali gharama za uzalishaji (Production cost) Vingi vilifeli mikononi mwa Nyerere mwenyewe! Na ilibidi vipewe ruzuku toka kwenye kodi.
Njaa ya miaka ya mwisho Sabini na Vita ya Uganda na Tz vilifirisi kabisa nchi. Nyerere akaenda kwa mabeberu kuomba mkopo
Walimpa masharti yafuatayo;
i. Kujiondoa serikali kuzalisha,kuagiza na kuingiza bidhaa. Iwe inakusanya Kodi tu.
ii.Kuwepo na soko huria. Bei za bidhaa zitokane na ushindani na mahitaji ya soko. (Serikali ijiondoe kupanga bei)
iii. Ashushe thamani ya shilingi
iv. Kuwepo uchangiaji katika huduma za kijamii baina ya serikali na wananchi ( Cost sharing) ili kuipunguzia mzigo serikali.
vi.Apunguze idadi ya watumishi wa umma na mishahara yao.
vii.Abinafsishe viwanda alivyopora na vile alivyopora.
Nyerere aliyakataa masharti huku akinukuliwa kwamba anayedhani Tz itayakubali masharti hayo ni mwendazimu akiwa ziarani Uingereza (Scotland?). Mwisho alienda Mara ya pili mezani IMF na WB wakasimama kwenye masharti yao.
Nchi ilikuwa taabani na Nyerere ikabidi ang'atuke kulinda msimamo na heshima yake.
Mwinyi akachukua nchi na kutekeleza masharti.