REDEEMER.
JF-Expert Member
- Feb 22, 2015
- 8,925
- 14,890
Mimi ni Mkenya mimi ndio najua historia ya Kenya. Wewe hujui asilimia ishirini ya ninachokijua kuhusu Kenya. Ninarudia, serikali ya Kenya inajua vizuri kwamba njaa hasa Nairobi itawang'oa mamlakani. Hebu nikupe mfano. Wakati wa serikali ya nusu mkate, yaani kati ya Raila na Kibaki, kulikuwa na uhaba wa unga na bei pia ilikuwa imepanda sana, nafikiri ilikuwa mwaka wa 2011. Watu walikuwa hawana unga si Turkana tu bali pia maeneo ya Town na Cities. Raila ambaye alikuwa waziri mkuu wakati huo ilibidi aambie watu jinsi atakavyoshusha bei ya unga, na kweli alivyosema serikali ilishusha bei na watu wakatulia. Hizo video zipo youtube. Pia 2017 kulikuwa na hio shida lakini serikali iliimport kutoka Mexico kwa hivyo Wakenya hawakuumia. Serikali walirekebisha bei ya unga. Unadhani njaa inajua Mkikuyu au Mjaluo?
Doh so kumbe chakula Kenya kinaweza kumpa mtu urais? Basi Kenya ni taifa la njaaa tena njaa kali