Viwanja ambavyo havistahili kuchezea mechi za ligi kuu

Viwanja ambavyo havistahili kuchezea mechi za ligi kuu

Viwanja ni vya CCM...na unajua tena mambo ya CCM..kwanza hivi ni vya kutaifishwa..upumbavu mtupu.

Au timu zingeteneze viwanja vyake maana hivi vya ccm hata vikiwekwa nyasi bandia bado vina matumizi mengi sana..itakuwa ni kupoteza tu muda.

Bodi ya ligi iache kulala..ligi inakuwa kwa kasi (ushawishi wise) huku viwanja vinaendelea kuwa utopolo.
 
Uwezekano huo mbona upo hata wapenzi na mashabiki wa mpira tu wanaweza kuchanishana wakaweka nyasi nzuri tatizo ni kwamba nani mmiliki wa hivyo viwanja?

Zaidi ya 70% ya viwanja vyote wanavimiliki CCM nadhani tuwashauri kwanza hawa watu
Vilabu lazima vijenge viwanja vyao, hili tatizo halitaisha
 
Leo ndio mnaona viwanja vibovu? Hivi Simba wanapofanyia mazoezi pale bunju uwanja ukoje?.

Tulipolalamika kuhusu viwanja wakati mnashinda mechi za mikoani hamkuona umuhimu wake

Leo kimeumana mnaanza kulia Lia twende hivyo hivyo kila mtu ashinde mechi zake Kama ambavyo mlikuwa mkisema miaka iliyopita.
 
Hakuna shabiki wa simba aliewahi kusema viwanja vya mikoani ni vizuri pamoja na kwamba simba ilikuwa inapata ushindi huko.
Fainali ya FA kule kigoma na sumbawanga zote zilipigiwa kelele humu na mashabiki wa simba kuhusu hivyo viwanja vibovu.

Viwanja vizuri ni kwa faida ya wote.
 
Hii nchi bwana tupo kwenye giza nene halafu unasikia kenge mmoja amepiga kama billions 5 hivi kirahisi tu huku wananchi tunakufa njaa
 
Azam wangelazimisha angalau 10% ya zile 223 billions kwenda kuweka artificial pitch kwenye viwanja vyote vya mikoani.

Viwanja bora vitaongeza thamani ya product especially in terms of sponsorships.

Watanzania ni watu wavivu sana kufikiria
Sio kazi ya Azam hiyo, tulishawashauri wenye viwanja na proposal kabisaaa.Vingi ni vya Chama Cha Mapinduzi ila sasa kusikia kwao ni hakuna na kuna siasa chungu mzima kule.

Sent from my SM-G9350 using JamiiForums mobile app
 
Back
Top Bottom