Viwanja vidogo vya ndege 208 vyafungiwa Tanzania baada ya kubainika kushindwa kufuata kanuni

Miss Zomboko

JF-Expert Member
Joined
May 18, 2014
Posts
4,618
Reaction score
9,611
Mkurugenzi mkuu wa Mamlaka ya Usafiri wa Anga Tanzania (TCAA), Hamza Johari ametangaza kuvifunga viwanja vidogo vya ndege 208 baada ya kubainika kushindwa kufuata kanuni ya 323 na kanuni nyingine za usafiri wa anga za viwanja vya ndege za mwaka 2017.

Amesema kanuni hizo zinakataza uendeshaji wa viwanja vya ndege bila kupata usajili au leseni inayotolewa na TCAA na ni kosa linaloadhibiwa kisheria.

Johari ametoa kauli hiyo leo Jumatatu Desemba 23, 2019 wakati akizungumza na wanahabari, akisema viwanja hivyo 208 vimeondolewa katika rejista ya viwanja vya ndege na havitaruhusiwa kutumika bila idhini ya TCAA.

"Tulifanya uhakiki wa miezi mitatu kwa kutumia ndege maalumu kuviangalia viwanja hivyo ambapo tumebaini ni mapori tu. Tuna viwanja vya ndege vidogo 643 kati hiyo 208 tumevifungia na tutaweka katazo," amesema Johari.

Johari amesema Mei 6, 2019 ilitoa muda hadi Desemba 31, 2019 kwa wamiliki au waendeshaji wote wa viwanja ndege vidogo kutimiza matakwa ya kanuni na kusajili au kupata leseni.

"Mamlaka inawapongeza wote walioitikia wito na imepokea maombi ya kuongeza muda hadi Machi 31 mwaka 2020 kwa wale waendeshaji wa viwanja vidogo 120 waliomba kwa ajili ya mchakato huu," amesema Johari.

Mwananchi
 
Hivyo viwanja vya ndege vipo Tanzania au?
 
Tutajie hivyo viwanja

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Angevitaja hivyo vilivofungiwa kwanza, kimfano mkoa mzima wa dodoma, viwanja vya ndege ninavovijua ni viwili tu. Kimoja kipo dodoma mjini kingine kipo wilaya ya kondoa.

Hivi kuna mkoa ktk tz hii una viwanja vya ndege zaidi ya kumi!?

Kasema kuna jumla ya viwanja zaidi ya 600.
Mikoa tuliyonayo haizidi 35.

Kwa idadi hiyo inabidi angalau kila mkoa uwe na viwanja sio chini ya 15.

Huyu mzee wa chato anawapeleka puta hata hawajielewi!

Vitakuwa ni airstrips

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Back
Top Bottom