Viyoyozi vya China vyakaribishwa na watu wa Ulaya kutokana na joto kali

Viyoyozi vya China vyakaribishwa na watu wa Ulaya kutokana na joto kali

Yoyo Zhou

Senior Member
Joined
Jun 16, 2020
Posts
199
Reaction score
322
VCG111651382039.jpg
Bara la Ulaya hivi karibuni limekumbwa na mawimbi ya joto kali. Inakadiriwa kuwa halijoto ya juu imesababisha vifo vya takriban watu 15,000, wengi wao wakiwa wazee wanaoishi katika nyumba zisizo na viyoyozi.

Takwimu zinaonyesha kuwa mwaka 2025, mauzo ya viyoyozi vya China barani Ulaya yaliongezeka kwa asilimia 39.5, na nafasi ya viyoyozi vya chapa za China kwenye soko la Ulaya iliongezeka kutoka asilimia 27 ya mwaka 2023 hadi asilimia 41 ya mwaka 2025. Joto kali la mwaka huu limeongeza nafasi hiyo kwa kasi zaidi.

Wakati huohuo, baadhi ya wanasiasa wa Umoja wa Ulaya wanaendelea kulalamikia suala la “nakisi ya biashara na China”. Timu za China na Umoja wa Ulaya hivi karibuni zilifanya mazungumzo kuhusu masuala ya kiuchumi na kibiashara, lakini upande wa Umoja huo haukuonesha nia ya dhati ya kushirikiana, ukirudia tena na tena kusisitiza nakisi ya biashara. Rais wa Tume ya Ulaya Ursula von der Leyen hata alitoa matamshi makali katika mkutano wa kilele wa Brussels, akidai kwamba Umoja wa Ulaya unaweza kuweka vikwazo mbalimbali dhidi ya China.

Kwa kweli, Umoja wa Ulaya hapo awali ulikuwa umeweka vikwazo vya ushuru dhidi ya viyoyozi vya China, kwa kisingizio cha kulinda mazingira. Hata hivyo, hatua hii ilishindwa kuongeza ushindani wa makampuni ya Ulaya. Kwa upande mwingine, makampuni ya China yalikamilisha teknolojia yake haraka, na ili kukidhi matakwa ya Umoja wa Ulaya.

Viyoyozi si mfano pekee katika uhusiano wa kibiashara kati ya China na Umoja wa Ulaya. Kutoka viyoyozi hadi paneli za jua, na kutoka betri za lithiamu hadi magari ya umeme, mauzo ya bidhaa za kijani zinazotengenezwa China barani Ulaya yanaendelea kuongezeka. Ursula von der Leyen amependekeza uchunguzi dhidi ya ruzuku kuhusu magari ya umeme ya China, akitaja hitaji la “kulinda viwanda vya ndani vya Ulaya”. Hata hivyo, ukweli ni kwamba magari ya umeme ya chapa za Ulaya hayawezi kushindana na yale ya China katika bei na ubora.

Kuchukulia nakisi ya biashara kama kwamba China inapata faida na Ulaya inakula hasara, ni dhana potofu na hatari. Kiini cha uhusiano wa kiuchumi na kibiashara kati ya China na Umoja wa Ulaya ni mahitaji ya soko. Ulaya inahitaji bidhaa bora na za bei nafuu ili kukidhi mahitaji ya watu wake na kufikia malengo yake ya kulinda mazingira, huku China ikiwa na uwezo wa uzalishaji na usambazaji wa bidhaa hizo unaotokana na minyororo kamili ya viwanda. Huu ni mpangilio wenye manufaa kwa pande zote kutokana na utandawazi wa uchumi duniani
 
Back
Top Bottom