Vladimir Putin amewataka wanajeshi wa Ukraine wajisalimishe wenyewe

Vladimir Putin amewataka wanajeshi wa Ukraine wajisalimishe wenyewe

Shing Yui

JF-Expert Member
Joined
Aug 8, 2015
Posts
15,168
Reaction score
38,049
Russia imewataka wanajeshi wa Ukraine wajisalimishe au waweke silaha zao chini warudi nyumbani.

Huku hayo yakiendelea kumesikika milipuko sehemu mbalimbali nchini Ukraine huku wanajeshi wengi wa Urusi wakitokea kila upande kuizunguka Ukraine. Wengine wanatokea nchi jirani ya Belarus kuelekea miji mingine ya Ukraine.

Uwanja wa kijeshi wa ndege mji mkuu Kiev umeshambuliwa, pia watu 7 wamekufa na wengine wengi hawajulikani walipo.

Urusi imesema inalenga maeneo ya kijeshi nchini Ukraine kwa kutumia silaha za kulenga shabaha za hali ya juu.
Screenshot_20220224-091826.png
Screenshot_20220224-091903.png
Screenshot_20220224-091931.png
Screenshot_20220224-091919.png
 
Huyu Putin ndiye Hitler wa sasa[emoji849]

Putin sio mzima kichwani - kama alivyokuwa Hitler. Itadhihirika muda sio mrefu.

Katika karne ya 21 kiongozi wa taifa kubwa kama Urusi hawezi kufanya uamuzi wa kipumbavu kiasi hicho usiokuwa na manufaa yeyote kwa taifa lake.

He’s gone completely nuts. Bado ana medieval mind set ya akina Alexander the Great na Gengis Khan!
 
Hitler wa kisasa anayetetea maslahi ya nchi yake

Putin ni fyatu. Urusi ina maslahi gani yatakayopatikana kwa kuisumbua Ukraine? Nani anahitaji utawala wa Putin huko Ukraine?

Anapoteza bilions of dollars huku nchi yake imerudi nyuma kiuchumi inategemea zaidi kuuza raw materials na silaha?

Hata China wanamcheka kinafiki.
 
Putin ni fyatu. Urusi ina maslahi gani yatakayopatikana kwa kuisumbua Ukraine? Nani anahitaji utawala wa Putin huko Ukraine...
Nani anamkubali wakati umeona mikoa miwili fastafasta imejitngaza kuungana na Urusi?

Ukitaka kujua maslahi ya Urusi kwa Ukraine tafuta historia. Urusi ipo tayari kufa na yeyote anayejaribu kuitengnisha na Ukraine
 
Putin sio mzima kichwani - kama alivyokuwa Hitler. Itadhihirika muda sio mrefu.

Katika karne ya 21 kiongozi wa taifa kubwa kama Urusi hawezi kufanya uamuzi wa kipumbavu kiasi hicho usiokuwa na manufaa yeyote kwa taifa lake.

He’s gone completely nuts. Bado ana medieval mind set ya akina Alexander the Great na Gengis Khan!
Hauna maslahi kwa taifa lake ?

NATO wanataka kukaa na silaha mlangoni kwako unaona sio maslahi ya urusi kujilinda .

Au unafikiri urusi ni zambia !
 
Putin ni fyatu. Urusi ina maslahi gani yatakayopatikana kwa kuisumbua Ukraine? Nani anahitaji utawala wa Putin huko Ukraine?

Anapoteza bilions of dollars huku nchi yake imerudi nyuma kiuchumi inategemea zaidi kuuza raw materials na silaha?

Hata China wanamcheka kinafiki.
Ukraine kujiunga nato ni tishio kwa usalama wa russia ..
Moscow ishafanya calculation zake ni bora kupoteza billions of money now kuliko anguko litakalokuja kutokea uko baadae wakiruhusu ukraine ijiunge na nato na kua kibaraka wa usa..
Usa anataka kuitumia ukraine kama kichaka cha karibu for their missions..
 
Nani anamkubali wakati umeona mikoa miwili fastafasta imejitngaza kuungana na Urusi?
Ukitaka kujua maslahi ya Urusi kwa Ukraine tafuta historia. Urusi ipo tayari kufa na yeyote anayejaribu kuitengnisha na Ukraine
Tatzo humu ndani watu wanamlaumu putin bila kujua sababu..
Afu nmegundua watz wengi hawajui vitu vingi wao kazi yao ni kusoma vichwa vya habar ya ulaya na us na kumlaum putin bila kujua hata chanzo ni nn...
Safi sana Putin.. wao si wahuni tuone sasa
 
Putin sio mzima kichwani - kama alivyokuwa Hitler. Itadhihirika muda sio mrefu.

Katika karne ya 21 kiongozi wa taifa kubwa kama Urusi hawezi kufanya uamuzi wa kipumbavu kiasi hicho usiokuwa na manufaa yeyote kwa taifa lake.

He’s gone completely nuts. Bado ana medieval mind set ya akina Alexander the Great na Gengis Khan!
Bila shaka maamuz aliyofanya Putin hayatofautian na maamuz aliyoyafanya Bush nchin Iraq na Afghanistan
 
Back
Top Bottom