STRUGGLE MAN
JF-Expert Member
- May 31, 2018
- 8,633
- 16,586
#EXTRAORDINARY - Moscow will retaliate if Sweden and Finland join #NATO! https://t.co/rfyczCteEJ
Follow along with the video below to see how to install our site as a web app on your home screen.
Note: This feature may not be available in some browsers.
Watanzania bhana kosa kuchoka smartphones duu !!!Putin ni fyatu. Urusi ina maslahi gani yatakayopatikana kwa kuisumbua Ukraine? Nani anahitaji utawala wa Putin huko Ukraine?
Anapoteza bilions of dollars huku nchi yake imerudi nyuma kiuchumi inategemea zaidi kuuza raw materials na silaha?
Hata China wanamcheka kinafiki.
[emoji1787][emoji1787][emoji1787][emoji1787][emoji1787][emoji1787][emoji1787][emoji1787][emoji1787][emoji1787][emoji1787]Shukran kwa kuongeza elimu hii muhimu. Kuna wengi hapa wanafikiri hii ni mechi ya mpira kati ya US na Urusi.
Inatakiwa wajue hii miamba inavyopima mambo yao. Putin angekuwa na UHAKIKA kuwa akivamia Ukraine basi US nao wanaingia vitani kikamilifu asingethubutu kuanzisha vita hiyo. Ingekuwa ni midahalo hadi kesho kutwa. Sasa anajua Marekani hawamtilii maanani kiasi hicho. Wamemuacha ajidunishe mwenyewe na watu wake hadi watie akili.
Sasa unasemaje Marekani kawaachia Ulaya NATO wakati huyu Marekani ni mwanachama wa NATO na mambo mengi kwa asilimia kubwa yeye ndo anayaendesha kwa kivuli cha NATO.. Anawaachia kivipi wakati anataka kutanua Base yake ya Kijeshi ndani ya Ulaya?Sio kweli. Fuatilia maoni ya Putin kuhusu makosa yaliyosababisha kuvunjika kwa USSR ndio utajua kero yake kubwa na harakati zake za kutaka kuifufua himaya ya Urusi kama ilivyokuwa. Ukraine ni moja ya jamii muhimu sana za taifa la Urusi.
Urusi sio tishio kubwa tena kwa Marekani. Silaha za nyuklia wote wanazo, kiuchumi Urusi imeshuka. China ndio tishio kubwa hata katika teknolojia zote inakuja kwa kasi zaidi wakati Urusi inachechemea.
Tangu kuisha kwa Cold War, Marekani imepunguza harakati zake Ulaya na kuwaachia EU na NATO. Inajishughulisha zaidi na masuala ya alqaeda na ISIS na inaumiza kichwa zaidi kuhusu China.
Of course Marekani imefanya ujinga mwingi katika kuvamia iraq, Afghanistan na hata zamani zile Vietnam. Lakini haijawa tatizo kwa Urusi huko Ukraine. Hilo ni zigo alilojitwisha Putin mwenyewe.
Ni juu yako kuamini kuwa Urusi ni tishio kwa US - leo hii. Let’s agree to differ.Sasa unasemaje Marekani kawaachia Ulaya NATO wakati huyu Marekani ni mwanachama wa NATO na mambo mengi kwa asilimia kubwa yeye ndo anayaendesha kwa kivuli cha NATO.. Anawaachia kivipi wakati anataka kutanua Base yake ya Kijeshi ndani ya Ulaya?
Urusi ina nguvu kwenye upande wa silaha za kivita na ndo biashara yake kubwa na urafiki wake na CHINA ndiyo unampa tabu Marekani..
Marekani anataka Ukraine wawe mwanachama wa NATO lakini URUSI hataki? Unajua kwanini? Ukraine akishakuwa mwanachama wa NATO Marekani ataendelea kujiwekeza kijeshi ndani yake. NA mwanachama yeyote wa NATO akishambuliwa ni sawa umetafuta VITA na NATO yote na ndo kitu PUTIN anakizuia kisitokee.
Hivi unajua Moscow iko Kilomita 450 toka mpaka na Ukraine na Kilomita 420 toka mpaka na BELARUS? Unajua kwanini URUSI ana-force urafiki na BELARUS na hata NATO wamesema BELARUS inatumika na URUSI kuipiga UKRAINE... Kwanini PUTIN asiwe na wasiwasi wakati Marekani tayari ina MAABARA ZA SILAHA ZA KIVITA ndani ya UKRAINE kwa siri?..
PUTIN anailinda MOSCOW na hata POPULATION kubwa ya URUSI ipo Magharibi ambako anapakana na BELARUS na UKRAINE, so lazima URUSI ahakikishe USALAMA wake kwa kuzi-control BELARUS na UKRAINE ili Marekani asizitumie dhidi yake...
Mfano mwingine ni kwanini Marekani yeye ndo yuko mstari wa mbele kuwasumbua IRAN na North Korea wakati nchi zenyewe HAZIMTISHI KUCHUMI? Ishu ni silaha za kivita na urafiki wao na URUSI na CHINA...
Marekani always wako macho na yeyote anayeonekana kuwa na nguvu fulani za kivita au kiuchumi asije kumpa shida katika harakati zake za kila siku za kuishika dunia.. Amejifunza kutoka kwa USSR ambayo ilijiamini sana yenyewe bila kuwa na washirika.
Naongelea Statistics na Reality, kuwa kwenye kila nyanja ya Umiliki na Utengenezaji wa Vifaa vya aina mbali mbali vya KIVITA na ULINZI, kwenye washindani wakubwa watatu wa dunia lazima wawepo USA na RUSSIANi juu yako kuamini kuwa Urusi ni tishio kwa US - leo hii. Let’s agree to differ.
Kwanza, elewa tu kuwa kiuchumi, kiteknolojia, kisilaha US iko top. Hakuna wa kuitisha duniani. Pili, hii vita iko zaidi ya flt kms 8000 toka Marekani. Tatu, baada ya kifo cha USSR na mwisho wa Cold War, Urusi imeshuka sana kwenye priorities za US; Putin anahaha kujithibitisha.
Nne, watu wa Ukraine wana nasaba kubwa na watu wa Urusi kuliko Wamarekani. Tano, China haina urafiki wa kweli na Urusi bali wa kimkakati kama ule ilio nao na North Korea. Sita, China baada ya kuwa na uchumi mkubwa wa pili duniani, ina interest kubwa na uhusiano wake na US na mataifa ya EU/NATO.
Pima mwenyewe, USA inapata hasara gani katika vita hii? Urusi inapata faida gani? Ukraine itaishia wapi? Dunia itanufaikaje?
Kwenye Aya ya Mwisho. Mimi naona kabisa mwisho wa Putin na Russia jeuri. Muda hauna kikomo. Kama utabiri wa kidunia unasema lazima kuje kuwa na serikali moja duniani. Watu kama Putin wasiopendwa ndani na nje ya nchi wakiwa kama kikwazo wataondolewa ndani na nje Hadi hapo wote tutakapokuwa na lengo sawa. Ndio atainuka Kiongozi mmoja tu wa dunia.Naongelea Statistics na Reality, kuwa kwenye kila nyanja ya Umiliki na Utengenezaji wa Vifaa vya aina mbali mbali vya KIVITA na ULINZI, kwenye washindani wakubwa watatu wa dunia lazima wawepo USA na RUSSIA
USA kama haioni USSR ni tishio asingehangaika kujenga maabara za kijeshi Ukraine na kama USA ingekuwa haitishiki na yeyote na inadharau nchi zingine kwa jinsi wewe unavyoona kwanini sasa atumie BAJETI KUBWA kusambaza MILITARY BASES dunia nzima?
Urafiki wa nchi na nchi tena wa haya mataifa makubwa hakuna wa kudumu na upo kimaslahi wote tunajua, but kwasasa CHINA, RUSSIA na NORTH KOREA ni marafiki na mimi ndo ninachosema kwakuwa ndo kilichopo kwa sasa...
Pamoja na USA kuwa top kwenye Uchumi, Teknolojia na kisilaha lakini hawezi kuridhika tu because wenzake pia hawalali, kwahiyo lazima na yeye aendelee kupigana kubaki pale alipo kwa kufanya kama anayofanya kila kukicha kudidimiza yeyote anayeonekana kuinuka...
Vita iko Kms 8000 toka Marekani, kama kawaida ya vita zote alizopigana na ndo lengo lake siku zote kuwa mtapigana naye lakini kwenye ardhi ya mtu mwingine ambaye ni Ukraine kwa sasa na ndo kitu Russia hakitaki yaani kuwe na BASE ya USA karibu naye.
Baada ya vita kwisha na baada ya Ukraine kubomolewa ndo tutaongelea faida na hasara... Tena naona USA na NATO yake watakavyohakikisha kummaliza PUTIN ili waje wajifanye wanatoa misaada kuitengeneza Ukraine wanayoshiriki kuibomoa kwasasa....
Mwamba mmoja anatishia dunia watu wametulia tuliii nawakubali San watu wa namna hii
"Venezuera.... korombia. .."we Mrusi aroo hebu nenda karee kande hii kitu sio revo yakoWamarekani walikuwa washajiandaa kuingia Venezuera, nini kilitokea baada ya mrusi kuingilia.
Tena walikuwa wanataka kusaidiwa na jeshi la korombia.
Kuna mtu humu amekomenti na kuogopa wakimbizi real
Unaizungumzia hii,View attachment 2130632
Hivo ndio unapenda kuona wewe unaye ona bora vita mailete refference za nyuma sisi tuna enda mbele tuzuie hivi vitu visitokee duniani havina ulazima tuzungumze Amani ya nini yote hii na ikiwa mtu ajachokozwa au kufanywa chochote watu hawaja lipiza wapewe uhuru haya mambo ya kitumwa mtu akitaka uhuru apewe sio kulazimisha kwa kumwaga damu kisa wewe una mabavu tuiombee Ukraine
Alikuepo jpm,Bongo tukija pata rahisi kama putin raha sana kina kenya kenya na Uganda yatakuwa makoloni et
Siyo kweli kwamba hawataki Vita..,.Lengo la NATO ni kupata wanachama ambao kwa mahitaji ya Kiulinzi/vita ikitokea kwa Maslahi ya Nchi kama Marekani au Uingereza basi huko nyuma Nchi mfano Ukraine utakuta wameweka Military Base ili iwe rahisi kwao kumuattack adui Yao...... Na hii ndicho Mrusi hataki kifanyike ni kama vile kukuwekea Adui yako Mlangoni kwa Nyumba yako. Jiulize kwa nini NATO wanataka Ukraine.....!!!!? Ni kujiandaa na Vita huko mbeleni, Kumbuka Marekani vita vingi hapigani kutoka Inchini kwake ni kutoka Military Base zake, kwanini Marekani ililalamika sana Cuba kujiunga na Urusi baada tu ya kupata Uhuru? The same applies to Ukraine.Watu hawataki vita. Hakuna alieufyata. Hakuna anaetaka kuanguka kwenye mtego wa huyo Schezophrenic Putin. Watu wanaangalia humanity kwanza. Hakuna anaemwogopa Putin. Sema watu wenye akili hawataki vita.
Vipi Bado unaamini huyo mpuuzi wenu Putin atashinda hii vita?Tunaendelea kula mtori pamoja na nyama sasa...
Kipindi Vladimir Putin akivuta bange zake uko ST. PetersburgRussia imewataka wanajeshi wa Ukraine wajisalimishe au waweke silaha zao chini warudi nyumbani.
Huku hayo yakiendelea kumesikika milipuko sehemu mbalimbali nchini Ukraine huku wanajeshi wengi wa Urusi wakitokea kila upande kuizunguka Ukraine. Wengine wanatokea nchi jirani ya Belarus kuelekea miji mingine ya Ukraine.
Uwanja wa kijeshi wa ndege mji mkuu Kiev umeshambuliwa, pia watu 7 wamekufa na wengine wengi hawajulikani walipo.
Urusi imesema inalenga maeneo ya kijeshi nchini Ukraine kwa kutumia silaha za kulenga shabaha za hali ya juu.
View attachment 2129602View attachment 2129601View attachment 2129604View attachment 2129605
mwanzoni si alisema atakae sogeza pua atapigwa na nuclear na silaha za radRussia imewataka wanajeshi wa Ukraine wajisalimishe au waweke silaha zao chini warudi nyumbani.
Huku hayo yakiendelea kumesikika milipuko sehemu mbalimbali nchini Ukraine huku wanajeshi wengi wa Urusi wakitokea kila upande kuizunguka Ukraine. Wengine wanatokea nchi jirani ya Belarus kuelekea miji mingine ya Ukraine.
Uwanja wa kijeshi wa ndege mji mkuu Kiev umeshambuliwa, pia watu 7 wamekufa na wengine wengi hawajulikani walipo.
Urusi imesema inalenga maeneo ya kijeshi nchini Ukraine kwa kutumia silaha za kulenga shabaha za hali ya juu.
View attachment 2129602View attachment 2129601View attachment 2129604View attachment 2129605
Huyu nae ni mbwa koko tu ambae ana Low IQ ndo maana a naonekana ni DICTATORmwanzoni si alisema atakae sogeza pua atapigwa na nuclear na silaha za rad