Halafu hii ya mtu kutangaza kugombea U-rais akiwa yuko nje ya nchi imekaaje? Ifike mahali tuweke kipengele kwenye Katiba kwamba mtu atatangaza kugombe U-rais akiwa ndani ya nchi, na kana atafanya hivyo akiwa nje ya nchi uchukuliwe kuwa ni uhaini! Na pia aruhusiwe kugombea akiwa tu amekuwa ndani ya nchi kwa kipindi kisichopungua miezi sita (6), kabla ya tarehe ya uchaguzi mkuu. Hii itasaidia kwa sababu kuna mtu anaweza akaondoka nchini akaenda akakaa huko nje halafu anarudi nchini miezi mitatu kabla ya uchaguzi, nia kuja kuvuruga uchaguzi tu halafu ukiissha anaondoka tena. Kwa hiyo mbali na kuwa raia wa JMT, anatakiwa pia awe amekuwepo nchini physically, angalau miezi sita kabla ya tarehe ya uchaguzi mkuu!
Hivi kwa mfano kwa mataifa makubwa kama Marekani, mtu anaweza akatangaza kugombea U-rais wa Marekani akiwa nje ya Marekani, kisa tu ni raia wa Marekani?