Bams
JF-Expert Member
- Oct 19, 2010
- 19,362
- 48,879
Kwani uliambiwa wameuziwa hayo madini au uliambiwa wamepewa bure?
Usijichanganye. Kwani SoutgbJirea ba Tanzania wameanza leo kukopeshana au wameanza leo kufanya biashara?
Nafikiri mleta mada ameleta kwa namna ambayo siyo sahihi.
Ninachoamini ni kuwa tumechukua mkopo kwa njia ya kawaida, yaani mkopo wenye riba. Mkopo hautakuwa na uhusiano wowote na rasilimali za nchi.
Halafu kumekuwa na makubaliano kuwa makapuni ya South Korea yaje kuwekeze kwenye sekta ya madini, ikimaanisha watakuja kufanya utafiti na wakiyapata hayo madini, watachimba kwa taratibu za kawaida kama kwa wachimbaji wengine ambao nchi zao hazijaipatia mkopo au zimetupatia mikopo. Wakikosa au wakiona sheria ni za hovyo, wataondoka. Lakini deni litabakia pale pale.
Ukweli ni kuwa hakuna mradi wowote wa madini ambao unaweza kusema kuwa Serikali i.efanya utafiti ikapata deposit ambayo resource yake imekuwa defined. Hivyo makapuni ya South Korea yakikubali kuja, yatalazimika kwanza kuwekeza kwenye utafiti, shughuli ambayo ina more than 90% possibility ya kupoteza hela yako.