Siku moja baada ya kutoa taarifa inayoeleza masharti ya mkopo ambao Tanzania imeupokea kutoka Korea Kusini hivi karibuni (Soma
hapa). Shiriki la Habari la Sauti ya Marekani (VoA) limeibuka na kutafuta ufafanuzi wa kina wa taarifa ya mkopo huo kutoka Serikalini. Habari hiyo inaeleza:
Serikali ya Tanzania imetolea ufafanuzi juu ya Mkopo waliopokea kutoka Korea Kusini ulioambatana na makubaliano ya ushirikiano katika Sekta ya Uvuvi pamoja na madini huku wachumi nchini wakiitaka Serikali kujenga utaratibu wa kutoa taarifa za kitaalamu Kabla ya kuingia kwenye Mikopo. Kueleza manufaa yatakayopatikana kutokana na Mikopo hiyo.
Mwandishi wa VoA anaripoti kuwa, kwa mujibu wa Msemaji wa Serikali Mobhare Matinyi amethibitisha Tanzania kuingia Mkataba na Korea Kusini, utakayoiwezesha Tanzania kupokea kiasi cha Dola za Kimarekani Bilioni 2.5 kwa Kipindi Cha Miaka mitano kuanzia 2024 mpaka 2028. Matinyi amesema kuwa Mkopo huo utaanza kulipwa baada ya miaka 25 na utalipwa kwa kipindi Cha Miaka 40.
Mkopo huo unatarajiwa kuwa wenye riba nafuu ya asilimia 0.01. Katika habari hiyo Msemaji wa Serikali ya Tanzania Mobhare Matinyi amesikika akisema
Mkopo huu utaanza kulipwa baada ya miaka 25 yaani ukifika mwaka wa 26 baada ya kuwa umemaliza kutolewa 2028. Tutapewa Kipindi Cha Miaka 40 kuulipa. Riba ya Mkopo huu ni 0.01%.
Tanzania kushirikiana na Korea kusini kujenga bandari ya uvuvi Bagamoyo
Aidha katika taarifa hiyo, anasikika Msemaji wa Serikali akisema hati za makubaliano zinajumuisha ushirikiano katika uchumi wa bluu, ikiwemo masuala ya Uvuvi na utafiti katika masuala ya madini ya kimkakati yakiwemo lithium na grafti. Makubaliano hayo pia yanatarajiwa kujumuisha ujenzi wa bandari ya Bagamoyo, mradibutakaogharimu Dola za Kimarekani milioni 156.5 ikiwa ni Moja ya sehemu ya mradi wa Jamhuri ya Muungano ya Tanzania ikishirikiana na Jamhuri ya Korea.
Hata hivyo Dkt. Bravious Kahyoza ambaye ni mchambuzi wa masuala ya uchumi amesema ni muhimu serikali kuweka utaratibu wa kufanya uchambuzi yakinifu kabla ya kuingia kwenye mikopo kuonyesha namna ambavyo taifa litakwenda kunufaika na mikopo hiyo.
“Serikali ni muhimu kuwa na utaratibu wa kufanya uchambuzi yakinifu na kuonyesha ni kitu gani kinakwenda kutokea, ni kwamba serikali ifanye uchanganuzi makini wa kuonyesha ni kitu gani tunakwenda kukifanya na kitakwenda kutoa matokeo gani kwa umma.” Amesema Kahyoza.
Matinyi amemalizia kwa kusisitiza mkopo huo ni mkopo nafuu na hauna mashariti yoyote yanayohusisha kutoa sehemu ya bahari na madini.
PIA SOMA
-
Prof. Kitila Mkumbo akanusha masharti ya Mkopo wa Korea Kusini. Asema utalipwa kwa miaka 40
-
VoA: Tanzania imepokea mkopo kutoka kwa Korea Kusini na kutoa sehemu ya bahari na madini
-
Ziara ya Rais Samia Korea Kusini atasaini Mkopo wa Tsh. Trilioni 6.51
-
Msemaji Mkuu wa Serikali, Mobhare Matinyi azungumza na waandishi wa habari kufafanua kuhusu Mkopo wa Korea Kusini