VOA: Zaidi ya Wanajeshi 80 wa Burkina Faso wauawa na Wanajihadi. Rais Traore akimbia Ikulu na kujificha ikihofiwa Uasi wa Jeshi

Inashangaza namna hawa magaidi walivyopata nguvu baada ya Marekani na Ufaransa kuondoa askari wao huko....
 
Kwanza jifunze kutofautisha ujamaa na Ukomunisti, pili nchi za Nordic sio za kijamaa, ni mixed economies ambapo kuna mfumo imara wa soko huria huku serikali ikitoa bure baadhi ya huduma muhimu na kuyajali zaidi makundi fulani muhimu.
Nimeshangaa sana jinsi alivyoandika kwa confidence
 
Tujifunze kitu Waafrica.
Ukianza kujifanya una akili nyingi kuliko wazungu jua kuwa umeyatimba.
Jpm aliwaita wazungu mabeberu nikaogopa hatima ya nchi yetu.Mugabe na degree zake 7 aliwafukuza wazungu mpaka leo hali ya uchumi wa Zimbabwe utafikili imejambiwa ushuzi wa nuksi.
Tukubali tu kuwa wazungu wana remote ya hatima ya maisha yetu huku Africa sema sisi watu weusi tupo kama kenge yaani hatuelewi mpaka damu puani itutoke.
Unakuta mtu anajiita msomi kwa kusoma vitabu vya NYAMBARI NYANGWINE alafu anaamini ipo siku mtoto ataweza mzaa mzazi wake inasikitisha sana.
 
Endeleeni kumsikiliza Mrusi kwa kujifanya mmechoka kuishi na wasterns
 
Huyu dogo anafanana moja kwa moja na Makonda akichukua nchi
 
Tutamkumbuka sana JPM na Job Ndugai.

Nchi inayotegemea mataifa ya nje kwa misaada haiwezi kuwa huru.

Misaada inatengeneza , ugaidi, ujangili ,kutorosha rasilimali za nchu, ushoga,usagaji na uasi pale tu serikali itakapoweza kuzuia pesa haram.
 
Kuna siku wazungu wataleta posa wakuoe, utasema nakubali tu, ntafanyaje sasa.
 
Kuna siku wazungu wataleta posa wakuoe, utasema nakubali tu, ntafanyaje sasa.
 
Nyerere kaachia madaraka mwaka 85. Nyinyi mliopo leo kinawashinda nini kuleta utajiri?



Wanadharau ujamaa ndio maana mchi inavamiwa na wajanja wanaojua nguvu ya ujamaa.

Hivi kwa mfano vijana wanaomaliza vyuo kama madaktari au walimu au watu wa kilimo wangefundishwa nguvu ya kuungana leo wasingepanga foleni kwenda kuomba ajira kwa wahindi na watu bonafsi bali wao ndio wangeajiri.

Mfano Walimu 12 wa masomo tofauti wanaweza kuanzisha Shule yao kwa kuanza kufundisha chini ya mti. Baadae wakaajiri Mhasibu na mtu wa HRM, walinzi, mapokezi ,mtu wa IT n.k. Wanachotakiwa ni kuwa na chaki na ubao tu. Shule kwa sasa ni biashara kubwa. Lakini wamepumbazwa na mabepari kwamba ni bora kila mtu aajiriwe atafute chake mwenyewe kupitia ujanja ujanja wake. Ujamaa ukiwa na watu waaminifu ndio mfumo sahihi wa Mwanadamu. Ubepari ni mfumo wa kishetani na kinyama. Mtu anaiba na kuwanyonya wengine ili akajenge nyumba yake binafsi na aweke ukuta mkubwa na kamera kila kona ,na mbwa wawili na mlinzi . Gharama ya ukuta ingetosha kujenga nyumba kwa mtu wa chini. Gharama ya Chakula cha mbwa kwa Mwezi ni kubwa kuliko mshahara wa walinzi wa umma au polisi . Yaani ameiba serikalini ,polisi wakakosa vitendea kazi au wakaajiriwa wachache na kushindwa kulinda jamii kwa sababu tu kuna majitu yanayoamini kazika kujenga mifumo yenye ubinafsi na kuiba mali za umma.

Madaktari Wanne wanaweza kuanzisha hospitali yao kwa kutibu kwa kuweka meza kwenye kordo .
Kinachotakiwa kwa wagonjwa no huduma inayotokana na ujuzi wao kwanza kiisha watu watalipa gharama za kumwona daktari.

Mwalimu Nyerere alikwamishwa na nchi za magharibi zilizomtengeneza iddi Amini akishirikiana nchi za Kiarabu kama Lbya na kisha kuivamia Tanzania.

Kwa mtu anayejua gharama ya vita anaweza kutafakari vita ya miaka miwili ni kwa kiasi ganiili ililigharimu nchi.
 
Huyu jamaa mimi ninapenda sana mwamko wake na imani yake kuwa raslimali za nchi yake ziwanufaishe watu wake. Rakini papara zake za kudhani kuwa dunia hii bado ina wakoloni na wakombozi naona zinampeleka pabaya. Mrusi hawezi kuja kuwa na moyo wa kukukomboa wewe mswahili huku anachinja ndugu zake huko Ukraine. Anachofanya na kutaka kutunihsiana na Magharibi lakini siyo kwa manufaa yako.

Katika dunia ya leo, huyu jamaa angefanya jambo la maana sana kama angewasimamia wawekezaji wa Magharibi wasitoroshe madini bila kuyalipia kodi badala ya kuwafyukuza na kuwaacha warusi wajichotee kwa kumpa ulinzi.
 
Hakuna kitu kinaitwa Ubepari wala wala ujamaa hizi sera mbili zilishachangamana na sasa tuna mixed economy ndio mfumo unao endesha dunia
Kwanza sio sera na mataifa mengi karibia 99% ya dunia kwa sasa ni ya kibepari, taifa lolote ambalo uchumi wake ni wa soko huria hilo ni taifa la kibepari.
 
Kwa ufupi Huelewi maana ya ujamaa, kujifunze kuhusu "command economy"
 
Inashangaza namna hawa magaidi walivyopata nguvu baada ya Marekani na Ufaransa kuondoa askari wao huko....
Kwani Hadi Marekani na Ufaransa kuja shida ilikuwa nini kama sio kuzuia kuenea Kwa hao hao Magadi?
 
Hata sisi ni suala la muda tu,hatuwezi kukubali ccm iendelee kuwa ndio alfa na omega wa taifa hili vizazi na vizazi.
 
Hivi huu uongo umeandikwa na RFI kweli?
Sema sishangai maana RFI ni redio ya ufaransa ambao ndio walikuwa wananyonya rasilimali za Burkina Faso bila kuzilipia
 
Kwanza jifunze kutofautisha ujamaa na Ukomunisti, pili nchi za Nordic sio za kijamaa, ni mixed economies ambapo kuna mfumo imara wa soko huria huku serikali ikitoa bure baadhi ya huduma muhimu na kuyajali zaidi makundi fulani muhimu.
Najua ni tofauti. Lakini ni aina mbili tofauti za ujamaa. Wote ni ujamaa tu, Kama ulutheri na ukatoliki ni aina za ukristo.
Au Ushiha na Usunni ni aina za uislam.

Kasome vizuri kuhusu historia ya Nordic countries socialism hasa miaka 1970 hadi 1990. Siasa yao ilikuwa conservative socialism.

Hiyo uliyo ita mixed economies wenyewe wanaita centerist socialism kwa maana ya mlengo wa kati lakini bado ni ujamaa. i.e. conservative and social democratic-led governments have moved toward the center.

Na kwa miaka ya karibuni nchi kadhaa watu wa social democratic wamechukua madaraka Ulaya.
Kutofanikiwa kiuchumi Tanzania ni zao la tabia zetu za asili uvivu, kukosa uaminifu, n.k.
Kwa ninyi msiojua ujamaa wa Nyerere ulikuwaje ngoja niwajuze. Kulikuwa hakuna wacheza kamali na pool table mitaani kutwa nzima au wapiga debe. Walikamatwa na kuwekea ndani kwanini wazurule badala ya kwenda kufanya kazi.
Kila mtu aliyefikisha miaka 18 alilipa kodi.
Matokeo yake yalionekana waziwazi. Fedha ya Tanzania haikuachwa mbali na Dola ya Marekani na huduma za kijamii nyingi zilipatikana kwa uhakika.
Tuliuza mazao ya biashara mengi nje ya nchi, n.k. Tuliokuwa na viwanda vingi tu.
CC: inamankusweke
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…