VOA: Zaidi ya Wanajeshi 80 wa Burkina Faso wauawa na Wanajihadi. Rais Traore akimbia Ikulu na kujificha ikihofiwa Uasi wa Jeshi

VOA: Zaidi ya Wanajeshi 80 wa Burkina Faso wauawa na Wanajihadi. Rais Traore akimbia Ikulu na kujificha ikihofiwa Uasi wa Jeshi

Trump alipotueleza ukweli tukasema katutukana. Hivi watu weusi Hasa Central /West Africa huwa wanataka nini??? Mara Jihad mara Uasi hivi hawawezi kabisa kuishi kwa amani??!!! Tumshukuru Sana Mwl JK nyerere Wallah kwa kutengeneza Foundation iliotuleta mpaka hapa tulipo
 
Ujamaa ni chachu ya umasikini,unaviza jitihada na kuficha wavivu kwenye kundi la wengi, ujamaa unazuwia ubunifu,vijiji vya ujamaa vya Nyerere viliirudisha jamii nyuma kimaendeleo,ikapunguza hata uzalishaji wa chakula,hivi tukiwauliza wafia ujamaa,lengo la ujamaa lilikua ni nini,mnaweza kusema!?..china imepiga hatua kipindi gani,Cha ujamaa au baada ya Deng kufanya reforms na kuachana na taboos za kijamaa?!..Afrika kusini haiwezi kuwa mfano wa kutetea ujamaa,na sababu ni dhahiri,na hata wakati huo wa ubaguzi,bado walikua mbele sawa tu au zaidi ya nchi za ulaya hata kisayansi na tech
Nordic countries (Dernmark, Sweden and Norway) ni nchi za kijamaa mbona hazijawa masikini Kama Tanzania?
Hawa walifanikiwa sababu ya uchapakazi (hardworking) na uaminifu(trust).

China wamefanikiwa na wanazidi kufanikiwa sababu ya uchapa kazi na uaminifu (trust) kwenye mambo mengi hasa mali za umma.

Kitu cha kushangaza wajamaa (USSR) ndio binadamu wa kwanza kupeleka spaceship kwenye outer orbit ikiwa na binadamu ndani. Wakati huo mabepari wanahangaika jinsi ya kuvusha spaceship kwenye anga la dunia.
 
Yuko wapi Sasa 😂😂
Sijui umefikiria Mara mbili kabla ya kuandika hivi!
Alikaa madarakani miaka mingapi?
Alileta maendeleo?
Nani walimuondoa madarakani na midege?
NATO walitumia article gani kwenye katiba yao kuivamia nchi ambayo haija ivamia nchi mwanachama wa NATO?
Huwezi kugundua tatizo au chanzo hapo ni nani?
Walipofanikiwa kumtoa madarakani nchi Sasa ipo katika Hali gani kiuchumi na kiusalama?
Hao waliomshambulia na midege ya kivita lengo waingize vibaraka wao waibe utajiri wa mafuta wa Libya na wamefanikiwa.
 
Unaandika kishabiki sana..andiko lako linakuwa biased..Unashanga BurkinaFaso mbona Congo hapo jirani kabisa wanauana kila siku???
Huyu ni wale Pro Western wanapenda kudanganywa na propoganda.

Burkino faso ipo safi kabisa hakuna lolote hizo ni propoganda za Western
 
Nordic countries (Dernmark, Sweden and Norway) ni nchi za kijamaa mbona hazijawa masikini Kama Tanzania?
Hawa walifanikiwa sababu ya uchapakazi (hardworking) na uaminifu(trust).

China wamefanikiwa na wanazidi kufanikiwa sababu ya uchapa kazi na uaminifu (trust) kwenye mambo mengi hasa mali za umma.

Kitu cha kushangaza wajamaa (USSR) ndio binadamu wa kwanza kupeleka spaceship kwenye outer orbit ikiwa na binadamu ndani. Wakati huo mabepari wanahangaika jinsi ya kuvusha spaceship kwenye anga la dunia.
Mifano mitatu katika nchi ngapi!?..isitoshe Sweden ujamaa ulifeli, Norway haikufanikiwa kisa ujamaa Bali uwekezaji kwenye nishati, uwekezaji ambao nabii wako wa ujamaa hapa hakuutaka, USSR ingefika mbali ikiwa wangeachana na ujamaa,lakini hata hivyo mwisho wa siku ilifeli na kuparaganyika
 
Huko Burkina Faso Hali inazidi kuwa tete Kwa bwana mdogo Rais Captain Ibrahim Traore ambae kwa Sasa anaishi Kwa kujificha ficha akihofia usalama wake.

Hali hii inajiri kuliwa na taarifa za Wanajeshi wengi wapatao 80-120 kuuwawa n wanamgambo wa jihadi hukunikidaiwa kwamba usalama wa Nchi hiyo unazidi kudorora na kwamba Baadhi ya kambi za Jeshi zimeasi kiasi ya kupelekea Rais Traore kutokomea kusikojulikana akihofia kuuwawa na kupinduliwa so anavuta mda Ili aweze kujadiliana na wanajeshi wanaodaiwa kiasi.

Washirika wa bwana Traore kina Wagner na Mali wanajaribu kumsaidia kadiri inavyowezekana Ili kuokoa jahazi.[emoji116][emoji116]
---

Hii ni taarifa ya RFI ambayo tunakutangazia Jumanne hii, Juni 18. Kati ya wanajeshi 80 na 120 wa Mali na mamluki wa kundi la Wagner kutoka Urusi wamewasili Ouagadougou katika siku za hivi karibuni. Hali ni ya wasiwasi nchini Burkina Faso tangu shambulio la Mansila siku ya Jumanne iliyopita Juni 11. Kiasi kwamba kikao cha Baraza la Mawaziri kilichokuwa kimeopangwa kufanyika siku ya Jumatano, Juni 19 asubuhi hakikufanyika tena.

Wakati wa shambulio la Mansila siku ya Jumanne Juni 11, zaidi ya askari mia moja wa Burkina Faso waliuawa na wengine kuchukuliwa mateka na wanajihadi wa JNIM (Kundi la linlodi kutetea Uislamu na Waislamu, lenye uhusiano na al-Qaeda). Kuhusu suala hili, mamlaka ya mpito ya Burkina Faso bado haijatoa tamko lolote na, baada ya mauaji haya, baadhi ya wanajeshi wameonyesha hasira yao.

Siku ya Jumatano ya wiki iliyopita, bomu lilirushwa katika makao makuu ya televisheni ya taifa. Chanzo cha tukio hilo kimeendelea kushangaza hadi leo. Kuhusu rais wa mpito, Kapteni Ibrahim Traoré, alionekana kwa kwa muda mchache siku ya Jumapili wakati wa swala ya Eid il Adha (Tabaski), bila kuzungumza. Hali ambayo inachochea tu maswali juu ya hali yake. Kikao cha Baraza la Mawaziri kilichokuwa kimeopangwa kufanyika Jumatano Juni 19 kwa hivyo hakikufanyika.

Kikao hiki kilipaswa kuongozwa, kama kila Jumatano asubuhi, na rais wa mpito, Kapteni Ibrahim Traoré. Lakini kikao cha Baraza la Mawaziri hakikufanyika. Hakuna taarifa rasmi, lakini chanzo katika ofisi ya rais wa Burkina Faso kinabaini kwamba kikao cha Baraza la Mawaziri kwa hakika lkimeahirishwa hadi kesho, Alhamisi, bila kutoa maelezo zaidi.
Ibrahim Traoré haojaonekana tangu wiki moja sasa

Kufutwa kwa kikao hiki au kuahirishwa hakutashindwa kuzua maswali kuhusu hali ya Kapteni Ibrahim Traoré, ambaye yuko kimya na hajaonekana tangu wiki moja sasa, na kuhusu kile ambacho kwa sasa kiko hatarini kwa mkuu wa mamlaka.

Siku ya Jumanne, Juni 18, katika taarifa kwa vyombo vya habari, jeshi la Burkina Faso kwa vyovyote vile lilitaka kuhakikisha: uvumi ambao umeripotiwa, tangu wiki iliyopita, "uvumi na uasi katika baadhi ya kambi za jeshi," kulingana na makao makuu ya jeshi, "havina msingi na vinapotosha”.

Mali imetuma wanajeshi 80 hadi 120 wa Mali na mamluki wa kundi la Wagner kutoka Urusi huko Ouagadougou kumsaidia rais wa mpito. Je, iddi hii ya wanajeshi na washirika wao wa Wagner zinahakikisha kwamba Kapteni Ibrahim Traoré anasalia madarakani? Je, ni suala la kuandaa aina ya "marekebisho ya mpito", kama baada ya mapinduzi ya pili ya kijeshi nchini Mali mnamo mwezi Mei 2021?

Katika makala iliyochapishwa alasiri ya leo, Gazeti la Le Monde linasema, kwa mujibu wa "duru za kuaminika", kwamba Ibrahim Traoré kwa sasa "amejificha" na kwamba "mazungumzo kati ya wanajeshi yanaendelea ili kuamua juu ya mustakabali wa utawala".

Chanzo: https://www.rfi.fr/sw/afrika/20240619-burkina-faso-kikao-cha-baraza-la-mawaziri-chaahirishwa-ibrahim-traoré-akimbilia-mafichoni?utm_medium=social&utm_campaign=x&utm_source=shorty&utm_slink=rfi.my/AhxU

My Take
Huyu dogo wa maigizo na kibaraka wa Russia hana miaka Mingi,alidhani yeye ni malaika? Mda utaleta majibu.
USA,France vs Russia=USA and France win.
 
Mifano mitatu katika nchi ngapi!?..isitoshe Sweden ujamaa ulifeli, Norway haikufanikiwa kisa ujamaa Bali uwekezaji kwenye nishati, uwekezaji ambao nabii wako wa ujamaa hapa hakuutaka, USSR ingefika mbali ikiwa wangeachana na ujamaa,lakini hata hivyo mwisho wa siku ilifeli na kuparaganyika
Hakuna kitu kinaitwa Ubepari wala wala ujamaa hizi sera mbili zilishachangamana na sasa tuna mixed economy ndio mfumo unao endesha dunia
 
Nordic countries (Dernmark, Sweden and Norway) ni nchi za kijamaa mbona hazijawa masikini Kama Tanzania?
Hawa walifanikiwa sababu ya uchapakazi (hardworking) na uaminifu(trust).
Kwanza jifunze kutofautisha ujamaa na Ukomunisti, pili nchi za Nordic sio za kijamaa, ni mixed economies ambapo kuna mfumo imara wa soko huria huku serikali ikitoa bure baadhi ya huduma muhimu na kuyajali zaidi makundi fulani muhimu.
 
Ujamaa ulikuwepo na bado upo Korea kaskazini,ubepari upo USA
Kaka unaweza kufafanua maana ya ubepari na maana ya ujamaa kinachotokea sasa hivi ni utofauti wa viwango vya kuaply hizo sera hakuna taifa linalo operate fully Capitalism ama Socialism
 
Kaka unaweza kufafanua maana ya ubepari na maana ya ujamaa kinachotokea sasa hivi ni utofauti wa viwango vya kuaply hizo sera hakuna taifa linalo operate fully Capitalism ama Socialism
Tofautisha capitalism na free market economy,free market economy ipo kitambo, capitalism ni wenye pesa kuilekeza serikali Cha kufanya,ndiyo ilivyo marekani,ndiyo maana palikua na maandamano juzi kati ya wamarekani kuitaka nchi yao toka kwa matajiri ambao ni 1% ya wamarekani
 
Kwakweli sijajua kwanini unasema Dogo wa maigizo, hivi ni lini Afrika tutapenda vyakwetu? huoni kwamba unatukosea waafrika wenzako? nafikiri ingalikuwa vyema kutafuta njia ya kutafuta ya jinsi ya kutatua matatizo yetu wenyewe? Kumpindua sio suluhisho bali kutafuta njia ya kutatua tatizo kwa kukubaliana wote kwa pamoja ndio njia njema. Tujipende na kulipenda bara letu.
Nyie ndiyo mnazidi kujichelewasha na kujipoteza na hiyo Africa yenu. Hapo Soth Africa tu wametema bungo na kuanua kumrudisha Kaburu, hala ninyi huko mnabaki kujitutumua na kudanganyana
 
Back
Top Bottom